Mbaga akisulubiwa na wananchi.
ENDELEA KUTIZA MATUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake.
Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo.
Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio.
Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye gari la polisi.
Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza.
MKAZI
mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita
alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu
wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota
Harrier, Ijumaa limeinyaka.
Shuhuda
wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Mbaga
na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba
power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari
aina ya Toyota Noah
“Lengo
lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop
lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.
Shuhuda
huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na
kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Mbali
na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na
kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.
HABARI NA GPL
No comments:
Post a Comment