Magari yakipita kwa shida katika mtaa wa Kasanga Kata ya Gerezani Kariakoo jijini Dar es Salaam kutokana na ufinyu wa eneo la kuegesha magari kutokana na eneo hilo kuzungukwa na ofisi nyingi pamoja na ofizi za Serikali.
Lori
lipita kwa shida katika mtaa wa Kasanga uliopo katika Kata ya Gerezani
Kariakoo jijini Dar es Salaam jana, hata hivyo wenye magari wanaoegesha
katika eneo hilo wameilalamikia Manisapaa ya Ilala kwa kuwatoza faini
kubwa kwa kuso la kuegesha vibaya.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kero ya maegesho ya magari.
Na Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, imetakiwa kuingilia kati na kupatia ufumbuzi kero ya maegesho ya magari kwenye mtaa wa Kasanga, eneo la Gerezani Kariakoo jijini Dar es Salaam badala ya kuwatoza wananchi faini kubwa kwa kosa la kuegesha vibaya.
Eneo hilo ambalo sehemu
kubwa ya majengo yake ni maghala ya kuhifadhia bidhaa na ofisi mbalimbali
ikiwemo ya NSSF kanda ya Ilala, imekuwa vigumu kwa magari kuingia na kutoka
kutokana na msongamano mkubwa wa magari yakiwemo malori.
Wenye magari
wanaofika kwa
shughuli mbalimbali kwenye eneo hilo, wamelalamika kutozwa faini na mawakala wa
Manispaa hiyo kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kuegesha vibaya magari.
Hata hivyo uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa waathirika wakubwa ni wateja wa NSSF
wanaofika kupata huduma kwenye ofisi hiyo kutokana na kuhangaika kutafuta
sehemu ya kuegesha magari na kushauri kuwa ni vema mfuko huo wa hifadhi ya
jamii ukatafuta sehemu nyingine ili kuweka ofisi hiyo.
“Kinachoniudhi ni jinsi
nilivyopata shida ya kuegesha gari langu, dada yangu nimemleta hapa ofisi ya
NSSF, ningeshauri ofisi hii wakaihamisha kutoka huku vichochoroni kwani eneo
hilo lina malori mengi na msongamano mkubwa wa magari na hawana sehemu yao ya
kutosha kwa wateja kuegesha magari” alisema Mohammed Abdallah.
Aidha halmashauri ya manispaa hiyo pia imelalamikiwa kutokana na
vitendo vya wakala wake, Tambaza auction mart, ambao ofisi zao ziko Manispaa ya
Kinondoni, Shekilango-Kumekucha, kwa kile kilichoelezwa ni tabia ya kuyakokota
magari na kuyapeleka kwenye yadi yao ili kupata fedha nyingi za adhabu ya
maegesho na hifadhi ya magari kwenye yadi hiyo.
“Mfano polisi hutoza shilingi elfu 30,000/= kwa kosa la
kuegesha vibaya inakuwaje kosa kama hilo, hawa jamaa wanadai 120,000/=?”
alihoji mwananchi mwingine ambaye ni muhanga wa adhabu hizo
Alisema, yeye wakati anakamatwa kwenye eneo hilo alikuwa ndani
ya gari akimsubiri mteja wake aliyeingia ofisi za NSSF, lakini maafisa hao
walimkamatwa na kumtoza faini ya shilingi 120,000.
Uchunguzi wa Nipashe umeonyesha faini kama hizo, halmashauri ya
manispaa ya Ilala huchukua shilingi 50,000/= na wakala wa kukamata magari
huchukua shilingi 60,000/=
Moja ya nakala ya risiti No IMC O34283 ya Novemba 12,
2013 iliyokatwa saa 5;42;55 ambayo ni ya Halmashauri ya Manispaa hiyo,
inaonyesha kupokea shilingi elfu 50 kama malipo ya faini ya kuvunja sheria
ndogondogo na risiti nyingine ni ile ya Tambaza Auction Mart No 0136/00003 ya
tarehe hiyo hiyo.
“Ukiangalia kwanza huu ni usumbufu na ni uharibifu mkubwa wa
magari, gari likamatwe Ilala, na Manispaa ya Ilala wana ofisi zao na yadi zao,
iweje gari hilo lipelekwe Kinodnoni, huu si usumbufu usio wa lazima kwa
wananchi” Mwananchi mwingine Yona Msamali alisema.
CHANZO: HABARI MSETO BLOG
CHANZO: HABARI MSETO BLOG



No comments:
Post a Comment