MWILI WA MAREHEMU DK SENGODO MVUNGI KUWASILI LEO,KUAGWA SIKU YA JUMAMOSI KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE


WAKATI  wananchi, ndugu, jamaa na marafiki wakiendelea kuusubiri mwili wa aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko  ya katiba marehemu Dk. Sengodo Mvungi kutoka Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu, viongozi mbali mbali wameendelea kuzungumzia utashi na ufanyaji kazi  wake enzi za uhai wake.
Akizungumza na 100.5 nyumbani kwa Marehemu Kibamba Jijini Dar es Salaam, Mwanadiplomasia ambaye pia ni mjumbe  wa tume ya mabadiliko ya  katiba Dkt.Salim Ahmed Salim, amesema wataikosa michango mingi ambayo alikuwa akiitoa marehemu katika mikutano yao.
Mwili wa marehemu Dr. Mvungi utawasili leo nchini na siku ya Jumamosi kutakuwa na ibada maalum ya marehemu  kwenye  Kanisa la Mt. Joseph  na baadaye  mwili wake utaagwa kwenye viwanja vya Karimjee kabla ya Jumapili kusafirishwa kwenda Kisangara Wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA CHINI


Mwanzoni mwa mwezi huu Dk Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi  nyumbani  kwake na alhamis iliyopita alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili  ya matibabu zaidi, hadi mauti yalipomfika
Wakati huo huo, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein hii leo  amemtumia  salamu za rambirambi  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba kufuatia kifo cha  Dk. Sengondo Mvungi.
Katika salamu zake hizo, Dk. Shein amemuelezea marehemu Dk. Mvungi kuwa ni mzalendo mwenye upendo mkubwa kwa nchi yake, mtaalamu wa sheria na  Vilevile mwanasiasa shupavu na makini,hivyo anamchango mkubwa sana katika taita lake.

No comments

Powered by Blogger.