Askari
wa kutuliza ghasia, FFU, wakipiga mabomu ya machozi hewani kuwatawanya
mashabiki wa Simba, waliokuwa wakifanya fujo kwa kung'oa viti na kurusha
uwanjani baada ya timu ya Kagera Sugar, kusawazisha bao lao kwa mkwaju
wa penati katika dakika ya 90+, iliyotolewa na mwamuzi, Mohamed
Theophile. Penati hiyo imepatikana baada ya beki wa Simba Joseph Owini,
kumchezea vibaya Daud Jumanne, penati hiyo iliyopigwa na Salum Kanon,
imezifanya timu hizo kutoka sare ya 1-1, wakati bao la SImba likifungwa
na Amis Tambwe katika dakika ya 45.
BAO
la beki wa kulia wa Kagera Sugar, Salum Kanoni lilipoteza amani ndani
ya Uwanja wa Taifa baada ya mashabiki wa Simba kuanza kung’oa viti hali
iliyosababiosha Polisi walipue mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo.
Kagera
ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Amisi Tambwe katika
kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa
njia ya panalti baada ya Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika
eneo la hatari.
Kwa
sare hiyo hali ya Simba imeendelea kuwa tyete kwani bado wamebaki
katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 21 nyuma ya Yanga yenye pointi 22
huku Azam na Mbeya City wakiwa juu kwa pointi 23 kila moja
wakitofautiana mabao ya kufunga.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa katika dakika zote kwani
timu hizo zilikuwa zikihitaji pointi tatu ili wajiweke sehemu nzuri
kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba
itamalizia mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Ashanti United mchezo
utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi ya Novemba 2.
Kipa
wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, akimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya
mwamuzi wa kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
Kipa
wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, na Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden,
wakimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati
katika dakika za majeruhi.
Wachezaji wa akiba wa Simba wakisikitika baada ya kuamuliwa kupigwa penati hiyo.
Askari wakiendelea kumdhibiti shabiki aliyekamatwa baada ya mashabiki hao kuvunja viti na kuanza kuruka uwanjani.
Askari wakiendelea kudhibiti vurugu..
Sehemu ya viti vilivyoharibiwa.
Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog
No comments:
Post a Comment