Kijana anonekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni (Kivuko) mbele kidogo baada ya Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari yake, huku abiria wengi wakiwa wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa.
Wasafiri
walipigwa butwaa zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na
huyu kijanda ndiye aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakati huo huo Kijana mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini
Hapa ni baada ya vijana hao kuzamia majini na wengine hawaonekani yanaonekana maji tu yanaruka wakati wao wapo chini ya maji hayo.
Ni zaidi ya Vijana 9 ambao wote walipanda Pantoni hiyo ya MV.MAGOGONI bila ulinzi wowote na baadae kupiga Mbizi wakitokea katika Pantoni hilo.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushangaza, kumemezuka tabia ya vijana
ambao wanashinda kakika kivuko kinacho unganisha Posta na Kigamboni
wakivizia kivuko hicho kinapopita kupanda na baadae kinapo ondoka hata
kikifika umbali mrefu wao kuanza kuruka na kupiga mbizi.
Mtandao
huu wa Dar es salaam yetu umekuwa ukifuatilia kwa kina swala hili na
kigundua kuwa hakuna mtu ambaye anawazuia vijana hawa wanaofanya mchezo
wa hatari, ingawa kwa upande wa pili kimekuwa ni kivutio kikubwa kwa
wale wasafiri..
Vijana
hawa ambao hawalipii hata kiasi kidogo katika kivuko hicho wameendelea
kuhatarisha maisha yao na pindi wakijua na kufahamu kabisa eneo ambalo
kivuko kinapita huwa ni sehemu ndefu sana ambayo inaweza kusababisha
madhara makubwa kwao na pengine kifo.
Hata hivyo inawezekana wahusika hawalijui hili au lah wanalijua lakini hawalizuii, hili ni jambo letu sote kujiuliza.



No comments:
Post a Comment