Wazazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mzee Kabwe Zuberi na Shida Salum.
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, jana alisindikizwa na wazazi wake pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari aliouitisha baada ya kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho. Tangu alipoanza kupata umaarufu katika medani ya siasa, mbunge huyo hajawahi kuonekana hadharani akiwa na baba yake mzazi, Zuberi Kabwe, bali mama yake Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Mbali ya wazazi hao, wasanii maarufu waliokuwapo
ni Peter Msechu, Selemani Msindi (Afande Sele), Mwasiti Almas, Mwanahawa
Abdul (Queen Darleen) na Clayton Revocatus (Baba Levo).
Wanamuziki hao ni miongoni mwa wanaounda kundi la Kigoma All Stars ambalo Zitto ametoa mchango mkubwa katika kuliendeleza.
ENDELE KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Pia kulikuwapo wakereketwa wa Chadema ambao baadhi
yao walimuuliza maswali. Mmoja wao alitaka Zitto aeleze ni kwa nini
alivitaka vyama vya siasa vipeleke hesabu kukaguliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alihoji kuwa kwa kuwa kiongozi huyo alikuwa ndiye
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), pia
Naibu Katibu Mkuu wa (Chadema), alikuwa na nafasi ya kuwaarifu wengine
ndani ya chama chake kabla ya kufika hatua ya kutoa tamko kwa umma.
Akijibu swali hilo, Zitto alisema licha ya kuwa
kufanya hivyo siyo utawala wa sheria na kutokutenda haki kwa vyama
vingine, pia aliwahi kulizungumzia mara kadhaa ndani ya vikao vya chama.
“Nendeni mkawaulize kama mpaka leo mimi ni mmoja
wa watu wanaotia saini utoaji wa fedha, nilijitoa baada ya kuona mambo
hayaendi vizuri na nikahoji bila majibu,” alisema.
MWANANCHI
MWANANCHI




No comments:
Post a Comment