Waombolezaji ndugu na jamaa wakitoa jeneza na aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa leo.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake Gangilonga Iringa leo kwa heshima za mwisho
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 |
| Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia akilia kwa uchungu
kushoto ni mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza. |
 |
| Askari akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo leo. |
 |
| Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christina Ishengoma kulia akimpa pole
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa kifo cha
aliyekuwa katibu wa CCM mkoa Bw Emanuel Mteming'ombe |
 |
| Meneja wa Tanroad mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa akisaini kitabu cha maombolezo leo |

 |
CHAMA cha mapinduzi
(CCM) mkoa wa Iringa kimepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa katibu
wa CCM mkoa Emanuel Mteming'ombe kufariki dunia usiku wa kuamkia leo
akiwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Akizungumza
na mtandao huu wa ww.francisgodwin.blogspot.com juu ya kifo hicho
katibu msaidizi mkoa wa Iringa Jimson Mhagama alisema kuwa
Mteming'ombe alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa figo na
athima
Alisema kuwa Mteming'ombe alikuwa amelazwa katika
Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa zaidi ya siku tatu sasa
akitibiwa .
Hata hivyo alisema kuwa maradhi hayo yalimfanya
kushindwa kufika ofisini toka Novemba 27 mwaka huu siku ambayo mkoa
wa Iringa ulipata kuhitimisha mbio za bendera .
Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kuwa kifo cha katibu
huyo kimeacha pigo kubwa kwa chama hasa ukizingatia kuwa mchango
wake ulikuwa ukihitajika sana katika uhai wa CCM mkoa wa Iringa.
Msambatavangu
alisema kuwa mazishi ya katibu huyo yanataraji kufanyika kesho
Desemba 20 katika kijiji kwake Mageha mjini Rujewa wilaya ya Mbarali
mkoa wa Mbeya .
Alisema kuwa miongoni mwa viongozi wa CCM
Taifa wanaotarajia kushiriki mazishi hayo ni pamoja na naibu katibu
mkuu wa CCM Mwingulu Nchemba na viongozi mbali mbali wa chama na
serikali kutoka ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa.
Msambatavangu
alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa itaendelea kumuenzi Mteming'ombe
kwa kuendeleza yale yote aliyeyatenda katika chama mkoa .
Huku
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akizungumzia
juu ya kifo hicho alisema kuwa alipokea kwa mshituko mkubwa taarifa
ya kifo hicho baada ya kupokea simu majira ya saa 8 usiku .
Kiponza
alisema kuwa CCM mkoa na taifa imempoteza kiongozi mchapakazi ambaye
katika uongozi wake alikuwa na ushirikiano mzuri kwa kila mmoja
bila kubagua .
Miongoni mwa viongozi wa chama na serikali
mkoa wa Iringa waliofika nyumbani kwa marehemu Gangilonga Iringa
kutoa heshima zao za mwisho jana ni pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa
Dr Christine Ishengoma, katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayub ,
meneja wa Tanroad mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa ,mjumbe wa NEC mkoa wa
Iringa Mahamud Madenge , kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa salim Asas,
kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri na wengine wengi
Mdogo
wa marehemu Bw James Mteming'ombe alisema kuwa marehemu alizaliwa
mwaka 1956 na kuwa ameacha mke mmoja na watoto watatu .CHANZO FRANSISGODWIN BLOG,
|
No comments:
Post a Comment