HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BREAKING NEWS: RAIS WA ZAMANI WA AFRIKA YA KUSINI MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA


Rais wa Afrika Kusini Jaccob Zuma atangaza kifo cha Nelson Mandela kilichotokea December 05, 2013 huko Johannesburg nchini Afika ya Kusini. Mzee Nelson Mandela alizaliwa July 18, 1918, in Mveso, Transkei, South Africa. 
Marehemu mzee Nelson Mandela amefariki akiwa na umri wa miaka 95  na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa jela kwa miaka 27
Mandela alikua anapokea matibabu ya homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Rais wa taifa hilo, Jacob Zuma , alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kua mwanawe wa kume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangi alipostaafu mwaka 2004.


Uongozi wa mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mzee Nelson Mandela

HABARI NA BBC SWAHILI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: