Mtoto wa Kiume’ Geez Mabovu anaewakilisha Doll South Iringa ameruhusiwa kutoka hospitalini alipolazwa December 27, baada ya kuanguka mara tatu kabla ya show aliyotakiwa kufanya na Songa na Jan B mjini Iringa.
Binamu wa Geez Mabovu aliyejitambulisha kwa jina la Choti, ameongea na Tovuti ya Times Fm kupitia simu ya rapper huyo na kueleza kuwa rapper huyo ameruhusiwa kutoka hospitali leo (December 31) baada kuonekana anaendelea vizuri.
“Geez yuko poa, ndo tumetoka hospitalini kama nusu saa iliyopita yani yuko fresh, yuko nyumbani kwao kwa baba yake anaweza akaongea na anaweza kufanya chochote. Sema tunaogopa tu kwa sababu kuna watu wanamsumbua wengi ndio maana simu hatutaki kumpa.”Ameeleza binamu yake Geez Mabovu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akisimulia kwa undani kuhusu sababu iliyopelekea rapper huyo kukimbizwa katika hospitali ya mkoa ya Iringa, amesema Mabovu alikuwa anaumwa tangu akiwa Dar es Salaam lakini alikuwa anatumia dawa za kutuliza maumivu na kuendelea na shughuli zake kama kawaida, na kwamba alipofika Iringa alifanyiwa party siku ya Christmas ambayo ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Amesema afya ya mabovu ilikuwa mbaya zaidi wakati akisubiri show na kupelekea kuanguka mara tatu huku akiendelea kusisitiza kuwa atafanya show hali iliyowalazimisha kuahirisha na kumpeleka hospitali ambapo aligundulika kuwa na ugonjwa wa malaria.
Msikilize hapa akielezea zaidi:
Source: Times Fm




No comments:
Post a Comment