Mi nimetoka mtaa wa pili hapo nshazinguana na
mademu flani walikuwa wanataka kuniletea za fesibuku nikawashtukia,
nikawachana, wamemaindi nikaona isiwe tabu, nikaachana na kibaa chao
ikabidi nije maskani tupige stori.
… Inakuwaje kwanza?
Uko fresh?
Us’konde wala nini mwanangu, naona kama nataka
kukuzingua vile, mi leo amani tu hapa, na sikuulizi mambo ya mwaka
unaoisha najua ulizingua watu sana mwaka huu, acha uende tugange yajayo.
Uongo?
Najua unaitaka hii stori ya mademu niliozinguana
nao mwanangu, ntakupa ila kwanza ngoja niwarushe wanangu wanaonisoma
deile ambao mwaka umeisha huku wakiendelea kunipiga tafu, kwa
kulifuatilia Zee kila linakokatiza.
ENDELEA KUSOMA STORI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA STORI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwanangu Eddy Seng wa Mabegi bila nauli, Fisi, Rioba, Makunga, hata wewe pia mwanangu Big Up, mwaka ushasepa, tugange yajayo.
Sasa hao mademu bwana mi siyo kwamba walikuwa
washkaji zangu wala nini, walikuwa ni watu tuliokutana nao fesbuku humu,
kila siku wananizingua mara Ooh, ..Zee ibuka kiwanjani kwetu tule gambe
na nini ... Mi nikawa nawakata stimu tu kwa kuwapigia stori za waifu.
...Si unajua zile...
Unafkiri wanakoma sasa, wakawa kama wanakomaa tu
hivi kwa kuweka picha zao za kujiseksisha, mara tutoke nini, sasa kila
nikiwaangalia nikawa kama nazimika hivi, watoto wakali kweli ujue?
Siku moja mtu mzima nikaona kwani nini? Siyo kesi,
ngoja nikajimiksi na watoto wazuri na mimi nioshe vumbi, ingawa
kiukweli mtoto mkali kuliko wote ni waifu wangu na ndiyo maana yuko homu
pale.
..ukiona vipi pigana...
Ila kilichokuwa kinanizingua kwa wale mademu
unajua kilikuwa nini, mara wako bichi, kesho wako kwenye hoteli kubwa
wanakula bata, mara keshokutwa unakuta statasi mtu yuko JK Eapoti
anasepa, nikaona watoto hawa siyo wale wa kutiana mawazo watakuwa fresh
ngoja wawe washkaji.
Maana kuna wale uswazi taipu ambaye dakika chache
baada ya kujuana simu inaisha krediti, mara itaibiwa, na keshokutwa
ataibiwa waleti na hela zote kaweka humo, mwisho mtu mzima unaanza kuona
ya kazi gani sasa, unasepa.
Sasa hawa walikuwa wamejipanga, siku ya kwanza
nikawaibukia, mwanangu kwanza sura zao na zile za kwenye fesibuku
...tofauti mwanangu, kidogo nitoke nduki ila nikajipa moyo kwamba si
wana, kwani wachumba, kwenye wana hata wangekuwa magorila ingekuwa fresh
tu.
Haya ikaja zamu ya gambe na kulipa bili, kila
kikiletwa kikaratasi unakuta wote wameomba ekschuzi wameenda toileti,
halafu zile gambe nilizokuwa naziona kwenye picha mbona kama hazifanani
nao? Kwani niliwakopesha? siku inayofuata nikaachana nikawaambia wanangu
hizi laifu feki za fesibuku zinawapoteza, kama vipi jipangeni kuna
mengi mapya na mazuri ya kufanya.
...Mnapotea!
Mwaka unakuja huu haina haja ya kujifeki,
ukijifeki ndiyo unafeki maisha yako na maisha yako yakiwa feki unafikiri
kuna nini tena mwanangu mwenyewe?
Mi nach’kua taim...
MWANANCHI




No comments:
Post a Comment