HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAREHEMU PENINA PHILIPO MSUYA APUMZISHWA KWA AMANI KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE USANGI MWANGA

 Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usangi Mwanga akisoma misa ya Kumuombea Marehemu Penina Philipo Msuya aliyefariki mjini Dar Es Salaam Mnamo tarehe 1 Disemba 2013 kwa ugonjwa wa Moyo na hatimaye kusafirishwa Hadi Kijijini Kwao Usangi Mwanga mkoani Kilimanjaro Juzi Jumanne kwaajili ya Mazishi yaliyofanyika Jana Jumatano
 Mmoja wa Ndugu wa Marehemu Penina Philipo Msuya akisoma historia fupi ya marehemu Penina wakati wa Misa ya Kumuombea iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Baadhi ya Watoto, Ndugu na Jamaa wa marehemu Penina Philipo Msuya wakiwa na majonzi ya kumpoteza mama yao mpendwa wakati wa Misa ya kumsalia marehemu iliyofanyika jana kijijini kwao Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
 Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Familia ya Marehemu Penina Philipo Msuya wakitoa heshima zao za mwisho kabla ya kwenda makaburini kwaajili ya kuupumzisha kwa amani mwili wa Marehemu Penina Msuya
 Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakiweka jeneza lenye mwili wa Marehemu Penina kwaajili ya kuupumzisha Katika Nyumba yake ya Milele.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Penina Msuya waliohudhuria katika mazishi yaliyofanyika jana Jumatano Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Watoto wa Marehemu Penina Philipo Msuya wakiweka Shada la Maua Juu ya Kaburi la Marehemu mama yao mpendwa wakati wa mazishi ya Marehemu Penina Philipo Msuya yaliyofanyika jana Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro
 Mchungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Usangi akiweka shada la maua juu ya kaburi la Marehemu Penina Philipo Msuya wakati wa Mazishi yaliyofanyika jana Jumatano huko Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
Baadhi ya Watoto, Ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu wakiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya kumaliza kuweka mashada ya maua juu ya kaburi la Marehemu Mpendwa wao Penina Philipo Msuya.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: