Ngiri ni
Mnyamapori mtukutu huwasumbua wakulima wa mihogo na viazi vitamu hivyo
hulazimika kuwindwa lakini huweza kukimbia kwa kasi kati ya kilometa 48 kwa saa
kwa urefu wa mita 200 mwendo ambao ni wa kasi zaidi kuliko wanariadha
yeyote duniani.
Ngiri ana pua
kubwa,macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi uliopinda au
ulionyooka.Huwa ana mwili mkubwa,miguu mifupi na nywele
zilizojiviringisha.Ana kwato nne kwa kila mguu,mbili ni kubwa za mbele
zikitumika kutembelea.
Ngiri huweza kuzaa
msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropic,lakini hasa misimu ya mvua.Ngiri
jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18 kisha ataanza kupata hedhi
kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba.Ngiri dume huweza kushiriki maswala ya
uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa uzao
mmoja,wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12waitwao vibwagala kasha kuachishwa
kunyonya,familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa
kujamiiana
Kitaalamu Ngiri
wanaopatikana hapa nchini wanaitwa Phacochoerus
africanus massaicus ambao.
Ngiri wana umbo
lenye manyoya machache na urefu wa mita 1.5,wanasimama kwa urefu wa kwenda juu
kwa kati ya sentimita 63.5 na 85 hadi mabegani pia wanawastani wa uzito wa kilo
45 hadi 75 kwa majike na kilo 60 hadi 150 kwa madume.
Miguu ya Ngili ina
mifupa migumu iliyounganishwa na misuli yenye nguvu ambayo hufanya kazi
ya kuchimba,kuruka na kukimbia kwa mlipuko kutokana na uwezo wa kukunjika na
kunyooka haraka.
Ili kupata mwendo
kasi wa juu Ngili hunyoosha kichwa mbele na mkia juu ili kuweza kuuweka mwili
sawa na kuimarisha mwendo asianguke.
Ngiri hawana tezi
za jasho hivyo hujipoza kwa kutumia maji au matope wakati wa joto kali.Pia
hutumia matope kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua.Zaidi matope
huzuia wasiathiriwe na inzi na wadudu.
Utalii hususani wa
wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.
CHANZO: MALIASILI ZETU



No comments:
Post a Comment