HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MUME AMCHINJA MKEWE KAMA KUKU WILAYANI KAHAMA.

MWANAMKE mmoja  aliyefahamika kwa  jina la  Kwezi  Seleli (20)  mkazi wa kijiji cha  Kalama,kata ya Uyogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga  ameuwawa  kwa kuchinjwa  sehemu za shingoni  na mume wake akiwa amelala usiku.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Evarist Mangalla  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo saa kumi alfajiri katika kijiji hicho  huku  akimtaja mwanamume aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Chalia Samweli (25).

Kwa mujibu wa Kamanda huyoa amesema kuwa mwanaume huyo alitumia panga kumuua mke wake  huku naye akifanya jaribio la kujia  kwa kunywa sumu aina ya Diazone  inayotumika kuogeshea mifugo ambapo hakufa alikuwa mahututi.

Aidha kamanda amesema   kuwa katika eneo la tukio kulikutwa panga  moja na kwamba chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa wa mauaji hayo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa kupatiwa matibabu.

CHANZO: DUNIA KIGANJANI BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: