Mwimbaji wa nyimbo za injili Toka nchini SomaliaMARY SINKALA atakaeshiriki katika tamasha la kristmas litakalofanyika Dodoma Des 25 ndani ya uwanja wa jamhuri
Na John Banda, Dodoma
Waimbaji wa nyimbo za injili watakaotumbuiza katika Tamasha la kusifu (Shangwe za Xmas) Dodoma kutoka Nje ya nchi waendelea kuongezeka.
Ni Baada ya mwimbaji kutoka Nchini Kenya TUMSIFU RUFUTU mwimbaji wa wimbo wa Mwambie Farao kuwa rasmi kwenye tamasha la Kristmas litakalofanyika Dodoma Tar 25.12.2013 katika uwanja wa Jamhuri, Hatima
mwingine aongezeka kutoka nchini Somaria Bi. MARY SINKALA mwenye wimbo wa Mkumbuke Muumba wako.
Tayali waimbaji hao wate wameshawataka wakazi wote wa mkoa huo na vitongoji vyake na watakaotoka nje kujiandaa kwani wao wamejiandaa vya kutosha na kwamba watawafundisha namna ya kumkumbuka muumba wao na jinsi ya kuelekea kaanani.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Shangwe hizo ambazo kwa sasa ni gumzo mkoani humo kutokana na kuandaliwa kwa umahili mkubwa na kampuni ya Liberty Promotion Company ya mjini humo tayali wakurugenzi wake wamewataka watu kuhudhuri kwa wingi kutokana na kiingilio kidogo kitakachomuwezesha kila mtu kukimudu cha 2000 kwa wakubwa na watoto 1000.
Kampuni hiyo imesema Dodoma imekuwa nyuma kwa muda mrefu hasa nyakati za Sikukuu za kidini na hivyo wamekusudia kukata kiu za wananchi mkoani humo kwa shangwe za kumuimbia na kumtukuza mungu kupitia
matamasha ya mara kwa mara kuanzia na KRISTMAS ya mwaka huu, huku wakiahidi kuibua vipaji vya chipukizi wengi.
Tamasha hilo litawaunganisha waimbaji toka ndani na nje ya nchi hasa wa mikoa ya DSM na Dodoma itakayobebwa na waimbaji toka makanisa mbalimbali na wachuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
No comments:
Post a Comment