HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » UCHUNGU WA ALOE VERA, FAIDA LUKUKI KIAFYA

Licha ya ladha yake chungu, mmea wa aloe vera ukilimwa kwenye rutuba sahihi, kutunzwa vizuri na kusindikwa kwa uangalifu huwa na faida nyingi kwani una vichocheo chekwa vinavyoua vimelea vya magonjwa kama bakteria, virusi na fangasi.
Mtandao wa Mediclinic unaeleza kuwa Aloevera, huchochea utengenezwaji wa chembechembe mpya na tishu mpya zenye afya. Hufanya mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri na kutuliza matatizo yanayoathiri mfumo wa fahamu. Huondoa sumu mwilini na kufanya utendaji kazi wa mwili urudi katika hali ya kawaida.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Pia, husaidia kujenga seli mpya baada ya majeraha ya moto, kujikata, michubuko, vidonda vya tumbo, kung’atwa na wadudu wakali na wanyama. Husaidia matatizo ya kutopata haja, pia maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo. Huondoa matatizo ya ngozi kama pumu ya ngozi (eczema), chunusi (acne) na fangasi.
Ni msaada kwenye umeng’enyaji wa chakula, kuongeza kinga ya mwili, kuondoa maumivu sehemu mbalimbali za mwili, matatizo ya usingizi, uchovu wa mwili usioeleweka, ugonjwa wa koo na pumu.
Hutibu matatizo ya kuhara na kutopata haja kubwa kiurahisi, hutibu sukari, vidonda vya tumbo. Wanaume wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kuziba kibofu cha mkojo na pia kinamama wanao sumbuliwa na uambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) ambayo huwafanya misuli ya kuzuia mkojo kulegea, mapafu, kusafisha maini na kuondoa sumu kwenye ngozi, aloe vera ni tiba.
Ili kupunguza uchungu, unaweza kutengeneza juisi yake na kuichanganya na asali ya nyuki wadogo.
Zimeandaliwa na Vicky Kimaro.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: