Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah akiwa ofisini kwake jana wakati wa mahojiano na mwandishi wa gazeti hili.Picha na Kelvin Matandiko
Dar es Salaam: Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na
mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema
tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.
Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.
Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge
hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na
ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.
“Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini,” alisema Dk Kashililah na kuongeza.
“Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini,” alisema Dk Kashililah na kuongeza.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akizungumzia safari ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya
upinzani, Freeman Mbowe nchini Uingereza, Dk Kashililah alisema Bunge
halina uwezo wa kumzuia mbunge yeyote kufanya shughuli zake safarini
baada ya kumaliza jukumu lililompeleka.
Dk Kashililah alisema Mbowe alikamilisha ziara
yake ya Bunge na kwamba baada ya hapo aliendelea na shughuli za chama
chake nchini humo.
“Suala hili lilikuwa limebeba hisia za kisiasa,
baada ya kusikika tu bungeni basi vyombo vya habari vikaanza kuwahukumu
wabunge ni mafisadi bila hata kutafuta ufafanuzi kutoka wetu. Sisi
taarifa hizo tulikuwa nazo kabla ya hata ya kuibuka bungeni, lakini
lilivyotafsiriwa sikupenda,” alisema Dk Kashililah.
Dk Kashililahb alisema, “Bunge lilikuwa limeratibu
jumla ya safari mbalimbali zilizokuwa zimependekezwa na Kamati 16,
lakini hazikufanikiwa kwenda zote kwa pamoja.
Alisema ziara zote za kamati huandaliwa kwa mujibu
wa kanuni ya 117 ambayo inazipatia mamlaka Kamati hizo kuandaa ziara
inazooana zina manufaa kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
MWANANCHI
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment