KLABU ya soko Arsenal ya nchini Uingereza,ipo tayari kutoa
Pauni Milioni 37 kumnunua Mjerumani ambaye wanaamini atakuwa Robin van
Persie mwingine.
Arsenal wanajiandaa kufika bei ya Julian Draxler, mwenye umri wa
miaka 20, ambaye ametambulishwa kama mlengwa mkuu kwa Gunners katika
usajili wa dirisha dogo baada ya kupita huku na kule kusaka vipaji.
Benchi la Ufundi la Arsene Wenger inaamini Draxler, ambaye anacheza
kama kiungo mshambuliaji katika klabu ya Schalke, anaweza kucheza kama
mshambuliaji pekee wa kati.
Arsenal wanaamini kuwa Draxler baada ya kusajili katika klabu hiyo
ataweza kuzipa pengo la Van Persie na Thierry Henry ambao waliwasili
klabu hiyo kama mawinga, lakini baadaye wakawa washambuliaji hatari.



No comments:
Post a Comment