HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » CHADEMA YAWATIMUA DK KITILA, MWIGAMBA


 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiandaa nyaraka za ushahidi dhidi ya viongozi waliofukuzwa kwenye chama hicho juzi, kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu. Picha na Fidelis Felix 

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewafukuza uanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo.
“Tumewavua uanachama kutokana na makosa ya kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013,” alisema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa mbele ya waandishi wa habari.
Wakati hayo yakifanyika, imeelezwa kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe ataendelea na  uanachama na ubunge kwa sababu ya mahakama, siyo kwa matakwa ya chama hicho.
Zitto ambaye alitajwa kuwa mhusika mkuu katika waraka huo amefungua kesi akiomba Mahakama Kuu izuie uanachama wake kujadiliwa hadi rufani yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama.  Hatima ya maombi hayo itajulikana leo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Maamuzi ya kikao
Akitangaza uamuzi wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema, “Kuhusu Zitto Kamati Kuu haikujadili wala kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.”
Huku akiyataja makosa 11 ya Zitto, Mwigamba na Dk Kitila yaliyotokana na waraka huo, Dk Slaa alisema, “Baada ya kumhoji Dk Mkumbo alikiri wazi kuwa Zitto alikuwa akiujua waraka huu ambao ulilenga kukiuka chama, kutengeneza tuhuma dhidi yangu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.”
Katika mkutano huo Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu alisema Zitto ataendelea kuwa mwanachama wa Chadema na mbunge kwa sababu ya  mahakama na siyo matakwa ya Chadema.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mwigamba na Dk Kitila, Novemba 22 mwaka jana walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu baada ya kukamatwa kwa waraka huo.
Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Dk Kitila, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho, huku Zitto akipendekezwa kuwania nafasi ya uenyekiti.
Utetezi wa watuhumiwa
Katika ufafanuzi wake kuhusu utetezi wa watuhumiwa, Dk Slaa alisema, “Dk Kitila pekee, ndiye alikuja kuhojiwa na Kamati Kuu iliyokutana Januari 3 hadi 4 na kwamba alikubali kuandaa waraka lakini alikataa kwa kuwa ulikiuka katiba na kanuni za chama. Pia alikataa kumtaja kwa jina mwandishi mwingine wa waraka huo anayetajwa kwa jina la M2.”

Alisema wakati wa mahojiano hayo, Dk Kitila alikiri wazi kuwa yeye na waandishi wenzake walimpa taarifa Zitto kuhusu mkakati huo na kwamba alikuwa anaufahamu. Hata hivyo, katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Novemba 22, mwaka jana, Zitto alisema kuwa alikuwa hajui chochote kuhusu waraka huo.
Alisema Dk Kitila alikataa kujadili hoja aliyoiibua kwamba Chadema kimebadili katiba yake na kuondoa ukomo wa uongozi.
“Pia Dk Kitila alieleza kuwa chama kinatumia fedha  ovyo, kikao kilitoa taarifa za fedha zilizojadiliwa katika vikao vilivyopita wakati yeye na Zitto wakiwa wajumbe, alionyeshwa michango ya fedha ya Jaffer Sabodo na ya watu wengine, ununuzi wa vifaa vya chama na jinsi mwenyekiti wa chama asivyohusika kuidhinisha matumizi ya fedha,” alisema.
Uamuzi wa Kamati Kuu
Alisema baada ya kumsikiliza Dk Kitila, Kamati Kuu imebaini kuwa mkakati huo haukulenga kumfanya Zitto kuwa mwenyekiti pekee, bali ulikuwa na malengo makubwa ya kukibomoa chama hicho.
“Ulilenga kukichafua chama, viongozi wake na kutumia tuhuma za uongo za ufisadi kwa sababu walifahamu kuwa chama chenye viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi hakiwezi kuaminiwa na wananchi,” alisema Dk Slaa.
Lissu amlipua Zitto
Kwa upande wake Lissu alisema Zitto alikihujumu chama hicho na kushiriki kujitoa kwa wagombea wake wa ubunge katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini, Singida Mjini na kuwa mwaka 2006, alipewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM).
Akijibu madai hayo, Zitto alisema hizo ni tuhuma mpya kama viongozi wa Chadema wanataka azijibu wamwandikie badala ya kupayuka kama kasuku.
Mwigamba, Dk Kitila wajibu
Kwa upande wake Dk Kitila Mkumbo alisema, “Sina pingamizi lolote kuhusiana na hatua ya kuvuliwa uanachama na kwa sasa natafakari hatima yangu kisiasa. Sipingi uamuzi nilijitetea lakini hawajaridhika na majibu yangu. Mimi ni muumini wa vyama vingi vya siasa, naamini iko siku nitajiunga na chama chochote, lakini ninachokifanya sasa ni kutafakari tu.”
Naye Mwigamba alisema hajashangazwa na kitendo cha kuvuliwa uanachama kwa kuwa tangu siku nyingi alijua uamuzi huo ungefanywa dhidi yake.
 “Acha waendelee na chama chao, nitaendelea kuamini  kilichoandikwa kwenye waraka, tulichokifanya katika waraka ule kililenga kukisaidia chama.


MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: