HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MWAKA 2013 NA VITUKO KATIKA SEKTA YA ELIMU


Mwaka 2013 ulianza kwa kushtua katika sekta ya elimu baada ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kutolewa Februari mwaka huu.
Matokeo hayo yaliibua mjadala mpana sana kuhusu mustakbali wa elimu nchini, ambapo asilimia 66 ya watahiniwa walipata daraja sifuri.
Mjadala huu ulitoa nafasi kwa Serikali na wananchi kukaa chini na kubaini nini cha kufanya ili kuinusuru sekta ya elimu.
Matokeo hayo yalikuwa ni mabaya ukilinganisha na mwaka mwaka 2009 ambapo jumla ya wanafunzi 195,000 sawa na asilimia 78 ya wahitimu wote walipata daraja sifuri na daraja la nne.
Pia mwaka 2010 wanafunzi 310,000 ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya wahitimu wote walipata madaraja hayo ya chini kabisa.
Uchunguzi wa matokeo
Baada ya matokeo ya mwaka huu, Serikali iliamua kuunda kikosi kazi cha kuchunguza chanzo cha matokeo hayo mabaya. Watanzania wengi walidhani hatua hiyo ingekuwa moja ya njia ya kuwapatia vyanzo vya kina kuhusu kufeli kwa wanafunzi.
Hata hivyo, badala yake Serikali ikatumia mapendekezo ya ripoti ya awali ya tume ya uchunguzi kufuta matokeo ya kidato cha nne yaliyokwishatangazwa.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Aidha, ililiamuru Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kuyachakata upya kwa kutumia mfumo wa zamani, kwa kisingizio kuwa mfumo mpya uliokuwa umetumika kutokuwa na maandalizi na wala haukuwa umefanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kutumika.
‘Daraja la tano’
Baada ya matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012, Serikali ilikuja na mkakati mwingine wa kubadilisha madaraja ya ufaulu.
Akitangaza mabadiliko hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome alisema hatua hiyo ilitokana na maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wadau wa elimu. Pamoja na mambo mengine, alisema Serikali imefuta daraja sifuri na badala yake kutakuwepo na daraja la tano.

Hata hivyo, katika kuonyesha kuweweseka kwa Serikali, kauli ya Mchome ilipingwa na mawaziri wake. Kwa mfano, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alinukuliwa akisema kuwa katika kubadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya sekondari, daraja sifuri litaendelea kuwepo.
Alisema dhana ya kuwepo kwa daraja la tano katika mfumo mpya, haikueleweka kwa wadau wengi na kwamba wataendelea kuelimisha umma juu ya mfumo huo mpya.
Naye Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi alisema taarifa aliyoitoa Mchome kuwa Serikali imefuta daraja sifuri kwa kidato cha nne na sita haikuwa ya serikali.
Kwa mujibu wa Lukuvi taarifa sahihi ilikuwa ile iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo.
Matokeo Makubwa Sasa
Agosti mwaka jana, Serikali ilitangaza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa upande wa elimu, ambao pamoja na mambo mengine unalenga kukuza kiwango cha ufaulu kwa wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne.
Mpango huo uliotangazwa na kila aina ya mbwembwe una mikakati tisa ya utekelezaji, ikiwamo upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza hadi ya mwisho na utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri.
Hata hivyo, mpango huu umekuwa ukitiliwa shaka kiutekelezaji kutokana na uzoefu wa Serikali kubuni mipango mingi ambayo mwishowe huishia katikati.
0754897287

MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: