HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » RAIS WA FIFA SEPP BLATTER ATANGAZA KUGOMBEA TENA MWAKANI


Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter ametangaza kwamba atatetea nafasi yake kwenye uchaguzi ujao mwakani.
Blatter alikuwa akidhaniwa kwamba angestaafu na tayari wanamichezo wengine walianza kufikiriwa kuchukua nafasi yake, lakini amekata mzizi wa fitna akisema anagombea kwa mara ya tano.
Blatter aliliambia gazeti la nchini mwake Uswisi la ‘Blick’ kuwa bado ataitaji muda zaidi ya kwakuwa bado ajamaliza majukumu yake.
“Mimi ni mgombea wa nafasi hii tena. Muda wangu unamalizika lakini kazi yangu niliyotaka kufanya bado,” alisema Blatter
Uchaguzi huo utafanyika katika makao makuu ya shirikisho hilo, Zurich nchini Uswisi Juni mwakani.
Makamu wa Rais wa Fifa, Jeffrey Webb na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Jerome Champagne wamekuwa wakitajwa kama mbadala wa Blatter lakini wote wamesema kwamba hawatasimama kushindana na rais wa sasa. Kiongozi wa Uefa, Michel Platini anadaiwa kutaka kumng’oa Blatter hapo Fifa, ili aingize mipango mipya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: