Bila shaka umeshakutana na tweets au picha kwenye Instagram inayoonesha upigaji kura wa tuzo za BET ambapo kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, Diamond anaonekana kuongoza. Well, ni good news kwa mashabiki wake lakini bad news ni kuwa kura hizo hazihusiki kabisa na kura zenyewe za BET kumpata mshindi.
Kituo cha redio cha V101.9 cha Marekani kimetengeneza utaratibu wake mwenyewe wa kuwapa nafasi wasikilizaji na wasomaji wake kumpigia kura msanii wanayempenda na kura hizo zitaishia kuwapa wao picha ya namna wasomaji wanapendekeza washindi wao. Kufanya hivyo ni rahisi sana na hata sisi tukiamua kutengeneza ballots systems kama hizi ingewezekana.
Utaratibu wa tuzo za BET upo tofauti kabisa na unaotumika kwenye tuzo zingine kama CHOAMVA ama MTV MAMA ambapo baada ya majina kutangazwa, mashabiki huwapigia kura wasanii wanaowapenda.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwenye tuzo za BET kuna jopo ama academy maalum yenye watu takriban 500 ambao ni wadau wa kiwanda cha muziki, habari na bloggers. BET huwataka watu hawa kupendekeza majina kwenye kila kipengele kwa mfumo wa kupiga kura ‘electronically’.
Kura hizi husimamiwa na kundi liitwalo “Yangaroo” ambalo hufanya kazi kwenye tuzo zingine pia. Kundi hili hupunguza majina na kubakiza wasanii watano kwenye kila kipengele na kuyatuma tena majina hayo (ambayo hutagazwa sasa rasmi kama majina ya mwaka husika) na kuyarudisha tena kwenye academy hiyo itakayopiga kura za mwisho kupata mshindi.
Habari njema ni kuwa, Vanessa Mdee pia ni miongoni mwa member wa academy hiyo. Hivyo bila wasiwasi atampigia Diamond. Haijulikani kuna members wangapi Afrika Mashariki ambao kiuzalendo watatakiwa kumpigia kura Diamond.
CHANZO: BONGO 5
CHANZO: BONGO 5
No comments:
Post a Comment