‘Happy’ ni wimbo uliopokelewa vizuri sana kote duniani kitu ambacho hata mwenye wimbo Pharrell aliwahi kutoa machozi ya furaha alipooneshwa video na Oprah ikionesha watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wamejirekodi video wakicheza wimbo huo.
Lakini huko Iran wimbo huo umewaponza baadhi ya mashabiki wa Pharrell ambao wamejikuta wakikamatwa na polisi kwa madai kuwa wamekiuka maadili ya nchi hiyo
Vijana wa Iran waliokamatwa
Video ya Wairan hao inawaonesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza ‘Happy’ kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa Iran wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita wakisherehekea na kujiburudisha kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya kukiuka maadili.
Hata hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtihani kwao.
“waliniambia kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana nikakubali kushiriki,” alisema mmoja wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.
Kulingana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13 walikamatwa kuhusiana na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa haijatangazwa rasmi.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu ambao umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea kukasirishwa na hatua ya vijana hao kukamatwa.
“yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,” alisema Pharrell katika ukurasa wake wa Facebook.
Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.
Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.
Kanda hiyo ya “Happy we are from Tehran” ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.
Hata hivyo inadaiwa kuwa vijana hao wameachiwa kwa dhamana jana Jumatano.
Mmoja wa vijana waliokuwa wamekamatwa pia jana alishare picha yake na kuandika,“Hi, I’m back. Thanks you @pharrell and everyone who cared about us love you all so much and missed you so much.
Chanzo: BBC





No comments:
Post a Comment