PICHA: BI HARUSI AAMUA KUMBURUZA SAKAFUNI MWANAYE WA MWEZI 1 JUU YA SHELA WAKATI WA KUINGIA KANISANI
Mwanamke mmoja wa Tennessee, Marekani hivi karibuni aliamua kufanya
kitendo ambacho huenda kwake aliamini kuwa ni ubunifu utakao wa ‘wow’
wageni waliohudhuria kanisani kushuhudia ndoa yake na mume wake
ikifungwa.
Mwanamke huyo aitwaye Shona Carter-Brooks aliingia
kanisani na mwanaye mwenye umri wa mwezi mmoja, lakini sio kwa kumpakata
mikononi kama ilivyotarajiwa na wengi, bali alimuweka kwenye mkia wa
shela yake na kumburuta katika sakafu ya kanisa wakati yeye na mume wake
walipokuwa wakiingia kanisani kuelekea kwenye ‘altar’.
Post a Comment