Jeneza lenye mwili wa marehemu Nasra Rashid likibebwa kuingiza katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro
ukitokea Dar es Salaam ambako mtoto huyo alilazwa kwa matibabu zaidi
kutokana na kuishi katika boksi kwa kipindi cha miaka minne tangu
kuzawaliwa kwake.
Mhudumu wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti akiwa amefungua jeneza ili kutoa mwili tayari kwa kuhifadhi katika jokofu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kutokana
na ratiba iliyotolewa na viongozi wa ustawi wa jamii mwili wa Nasra
utatarajiwa kuwasiri uwanja wa jamhuri kuanzia majira ya saa 2 asubuhi
na wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake watapata fursa ya
kuaga kisha saa 5 asubuhi hiyo hiyo msafara utaelekea katika makaburi ya
Kolla kwa ajili ya mazishi. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Jole Bendera anatarajia kuwaongoza wananchi kuaga mwili huo.
Mama
Mlezi wa Nasra Josephine Joel na Mwandishi wa habari wa gazeti la
habarileo Agnes Haule wakiwa kwenye huzuni mara baada ya mwili huo
kuhifadhi katika chumba cha maiti.PICHA/MTANDA BLOG
Baba mzazi wa Nasra (aliyeshika shavu) Rashid Mvungi akisikiliza jambo eneo la uwanja wa chumba cha kuhifadhia maiti.
Hapa akionekana mwenye huzuni kutokana na tukio hilo.
Mama Mlezi wa Nasra Josephine Joel akizungumza jambo na waandishi wa habari.
Akiteremka katika gari baada ya msafara uliobeba mwili wa marehemu mtoto wake Nasra kuwasili eneo hilo.
Mtoto
Nasra Rashid Mvungi (4), aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne,
amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa
zake za mwisho za uhai wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje
kunichukua”.
Nasra
ambaye alikuwa akitibiwa MNH, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana
baada ya hali yake kubadilika Alhamisi iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa
katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) ambako aliwekewa mashine ya
kumsaidia kupata hewa ya oksijeni.
Mama mlezi wa Nasra, Josephine
Joel alisema kabla hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa
kuzungumza maneno mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada
maalumu.
“Sitaki waje kunichukua, sitaki, sitaki, wasije
kunichukua, bibi Nasra umesikia,” ni maneno aliyokariri mlezi huyo
ambayo yalikuwa yakirudiwarudiwa na Nasra saa chache kabla ya hajawa
mahututi na kupelekwa ICU.
Josephine alisema mtoto huyo pia kila
mara alikuwa akidai apewe chips na soda na kwamba hadi mauti yalipomkuta
alikuwa akitibiwa maradhi ya homa ya mapafu ‘nemonia’.
“Nasra
alifariki saa 7.30 usiku, tangu Alhamisi iliyopita hali yake ilibadilika
na kuwa mbaya na imeendelea kuwa hivyo hadi alipofariki dunia,” alisema
na kuongeza:
“Bado niko Muhimbili nawasubiri watu wa ustawi wa
Jamii kutoka Morogoro wao ndiyo watakuwa na uamuzi kuhusu mazishi ya
mtoto huyo,” alisema.
Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Eligaeshi
alithibitisha kifo cha mtoto huyo, ambaye alipokewa hospitalini hapo Mei
26 mwaka huu akitokea Morogoro na kwamba hali yake ilibadilika ghafla
juzi saa 2:00 usiku.
“Jitihada za madaktari zilifikia kikomo saa 7:30 usiku, baada ya mtoto huyo kupoteza maisha,” alisema.
Kuzikwa kishujaa
Ofisa
ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti amsema kuwa mazishi
ya Nasra yatatanguliwa na ibada itakayoambatana na utoaji wa heshima za
mwisho katika Uwanja wa Jamhuri kesho, hatua ambayo alisema inatokana na
baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi kuwa mmoja wa watuhumiwa wa
mateso yake.
No comments:
Post a Comment