HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » POLISI WA USALAMA BARABARANI NA SUMATRA WAONGEA NA MADEREVA KWENYE KITUO KIPYA CHA MABASI CHA MAKUMBUSHO

 Askari wa usalama barabarani, Kinondoni, wakitoa maelezo kwa madereva wanaofanya safari za Makumbusho-Bagamoyo.
Wadau wameongea kuhusu kuhamishwa kwa kituo cha mabasi ya daladala kutoka Mwenge kwenda Makumbusho ambapo malalamiko yanahusu umbali wa kituo hicho kutoka maeneo ya abiria wengi na ubovu wa miundo mbinu sehemu hiyo kama ukosefu wa vyoo, vifaa vya kutupia uchafu na mashimo kwenye barabara kituoni na zile zinazoingia hapo.
 Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki, Conrad Shio (kulia) akizungumzia kuhamishwa kwa kituo cha Mwenge kwenda Makumbusho.
Malalamiko mengine ni kwamba kituo ni kidogo mno, hakina alama muhimu za kuonyesha mabasi yanakokwenda.  Wengi walitaka barabara za hapo ziwekwe lami,  na wengine wakataka nauli ya kutoka Bagamoyo iongezwe kwani mabasi sasa hayaishii Mwenge bali Makumbusho.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Mwenyekiti wa soko la Makumbusho, Bi Mary John (kulia), akiongea na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, SP Awadhi  Haji (kati), na Mkuu wa Usalama Barabarani, Kituo cha Kinondoni, Solomon Mwangamilo (kushoto).
 Mmoja wa madereva wa daladala akiuliza swali kwa viongozi wa usalama barabarani (hawako pichani).
 Askari wa usalama barabarani wakiwa katika kituo kipya cha Makumbusho ili kutoa ushauri na miongozo.
  Mwonekano wa kituo kipya cha Makumbusho.

PICHA NA GPL

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: