HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WAKULIMA WANAMDAI MWEKEZAJI MILONI 703 ALIZOWAKOPA ZABIBU TANGU MWAKA JANA MKOANI DODOMA

 Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wakulima wa Zao la Zabibu wanaomdai muwekezaji wa kiwanda cha Cetawico kinachowakopa zabibu zao na kushindwa kuwalipa kwa wakati ambapo kwa misimu miwili muwekezaji huyo anadaiwa zaidi ya 700. mil. waliokaa kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Dodoma Mhe. Hezekiah Chibulunje na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Hombolo Bwawani Jerad Mtagwa
 Mkulima na mkazi wa kijiji cha Hombolo Dodoma Wile Kaluganya akiongea jambo wakati alipokuwa akuliza jambo kwa Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi hayupo pichani wakati alipowatembelea ili kusikiliza malalamiko ya madai yao wanayomdai mwekezaji wa kiwanda cha Cetawico kinachonunua zabibu za wakulima hao.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI 

Mmoja wa wakulima wa zabibu Joseph Sanka akiuliza jambo kwa waziri, wakati wakulima wa Zao la Zabibu walipokusanyika na kutaka kujua ni lini watalipwa 700. MIL wanazomdai muwekezaji wa kiwanda  cha kutengeneza Wine cha Cetawico kutokana na kutowalipa fedha zao zaidi ya milioni 700 za tangu mwaka jana.
 Ofisa Tarafa wa tarafa ya Hombolo Isaac Songoro Akizungumza jambo Mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Dr David Malole, Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Dodoma Hezekiah Chibulunje na viongozi wengine wa Serekali, namnamuwekezaji wa Kiwanda cha kutengeneza Wine cha Cetawico asivyo na ushirikiano na viongozi wa Selikari.
 Mhasibu wa kiwanda cha Cetawico Jackison Temu akimsomea idadi ya madeni wanayodaiwa na wakulima Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Godfrey Zambi na viongozi wengine waliofika Kiwandani hapo
kutaka kujua ni kwa nini Muwekezaji wa Kiwanda hicho ameshindwa kuwalipa wakulima fedha zao kwa wakati.
Wakulima wa zao la Zabibu wa kijiji cha Hombolo wakiwa wamekusanyika walipokuwa wakimsikliza Naibu Waziri wa Kilimo Godfrey Zambi aliyefika kusikiliza madai ya madeni yao kwa muwekezaji wa kiwanda cha Cetawico anayedaiwa zaidi ya 700 mil. na wakilima hao.

Na John Banda, Dodoma
WAKULIMA wa zao la zabibu katika kijiji cha hombolo Wameitaka serekali kuwasimamia ili waweze kulipwa madai yao ya zaidi ya milioni 700 wanazomdai muwekezaji wa kiwanda cha Cetawico na baada ya hapo afukuzwe  kutokana kuzarau wazawa. Wakulima hao waliofikisha malalamiko yao mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi aliyefika katika kjiji hicho cha Hombolo Manispaa  ya Dodoma ili kusikiliza kilio chao.
Katibu wa ushirika wa Wakulima wa zabibu na Masoko hombolo Ramadan Mkombozi alisema wanamdai muwekezaji wa kiwanda hicho cha Cetawico Dr Florenzo Chesini Raia wa Italy 700 milion kwa zaidi ya miezi 9 hali inayowasababishi ugumu kimaisha kutokana na wengi wao kushindwa kulipa mikopo.
Alisema pamoja na jitihada mbalimbali walizofanya zikiwemo kushirikisha serekali ya wilaya na mkoa ili kuwasaidiwa kudai madeniyao bado wamegonga mwamba kutokana na kutopewa  ushirikiano na badala yake kuishia kupewa majibu yasiyoridhisha. ‘’Mhe. Naibu Waziri kwa kuwa umekuja tunaweza kupata madai yetu lakini huyu muwekezaji hii siyom mara yake ya kwanza kutotulipa hata mwaka jana msimu wa mwezi wa pili ilibidi Waziri Chiza aingilie kati ndiyo tukalipwa japo si malipo yote, tunachoomba ni bora aondolewe ili
aletwe mwingine atakaeshirikina na sisi vizuri,
Hata bei yenyewe si nzuri kwa sababu akipekewa Zabibu huwa zinapimwa tunaziacha na bei anapanga yeye kwa kiangazi analipa kilo moja tsh 800 au 1000 wakati masika 500 au 400 bila kujali Gharama za uendeshaji hali inayotupa hasara mara kwa mara  na mtu akihoji anaambiwa asipeleke tena, nasi hatuna pa kupeleka kutokana na kutokuwepo na
viwanda vingine’’, alisema
Awali Mhasibu wa kiwanda cha Cetawico Jacson Temu alimwambia Naibu Waziri Kilimo,Chakula na Ushirika Godfrey Zambi aliyefika kutaka kujua kiasi wakulima hao wanachodai kuwa ni 703. Mil ambazo Muwekezaji andaiwa na wakulima.
Baada ya maelezo ya Mhasibu huyo Ndipo Naibu Waziri huyo alipomuagiza kumfikishia ujumbe Bosi wake kuwa ahakikishe ndani ya mwezi huu wa sita wakulima hao wanalipwa fedha zao zote la sivyo serekali itachukua hatua

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: