HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » ZITAMBUE SABABU ZA WANAUME KUOTA MATITI

Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kamaglandular tissue.


Ni nadra kujitokeza, lakini kwa siku za karibuni baadhi ya wanaume wana maziwa kama walivyo wanawake. Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto wa kiume limekuwa kubwa katika dunia ya leo.
Inawezekana wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti tena makubwa ambapo watu wengi  huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu, tatizo hilo hujulikanakama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titiinayojulikana kama glandular tissue. Tatizo hili huonekana zaidi kwa watotowachanga na  wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

Ukubwa wa tatizo Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo hili la kukua kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu kama, transient gynecomastia kutokana nakuwepo kwa kichocheo cha aina ya estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wamama. Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri wa kubalehe  imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na  kuwepo kwa wingi kwa kimeng'enyo aina ya estradiol. Mara nyingi huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 17.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa natatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa kichocheo aina ya testosterone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki chatestosteron kutoka kwenye korodani ziazoanza kuzeeka. Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testosteron hutengenezwa katika korodani. Kichochezi cha testosteronndicho kichochezi kikuu cha kiume kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.

Nini hutokea?

Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kitaalamu kama, estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewakwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi yakawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu. 
Kichocheo hiki husababisha chembechembe zinazojulikana kama ductal epitheliakuongezeka kwa wingi, kurefuka na kugawanyika, kuongezeka kwachembechembe za mafuta na kuongezeka kwa mfumo wa damu kwenye matitihutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya testosteron na androgen kwa kutumiakimeng'enyo kinachojulikana kama

aromatase.

Aina za tatizo hili

-Puffy nipples -Kuongezeka ukubwa wachuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular.

-Pure glandular gynecomastia - Huonekanazaidi kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili, kutokana na matumizi yadawa za kujenga mwili ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha kichocheo aina yatesterone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen.

Kwa wanaume wembamba, tatizo hili hutokea kutokana na kuongezeka kwa tishu za tezi za maziwa (breast tissue gland) pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose.

Ni nani aliyeko  hatarini?

1.Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50. 

2.-Wenye uzito uliopitiliza

3.Unywaji pombe kupindukia

4.Magonjwa sugu ya figo au ya ini

5.Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika

familia.


Visababishi vya kukua kwa matiti kwa wanaume

-Pseudogynecomastia - Kuongezeka kwatishu zinazozunguka chuchu za matiti na huambatana na kuwepo kwa wingi watishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye virutubisho sahihi huondosha tatizo hili.



-Unilateral/asymetrical gynecomastia - Ni kuongezeka kwa titi moja pekee au la upande mmoja wa mwili wa mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. Titi la upande wa pili huwa kwenye umbile na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni kuongezeka kwa matiti yote mawili.


-Hypogonadism - Kutofanya kazi kwa korodani vizuri  na kuwa ndogo. Hii

husababishwa na magonjwa mbalimbali.

-Umri - Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili kutokana na kutolewa kwa

uchache   kwa kichocheo cha testerone na kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza kwa wingi kwa kimeng'enyo aina ya estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya testerone.

Pia, mabadiliko ya mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.

-Uzito uliopitiliza - Watu wenye uzitouliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen mwilini mwao na wakati huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya testerone.

-Saratani - Baadhi ya saratani kama vile ya kwenye korodani, tezi lililo juu ya figo, saratani ya tezi la kichwa, huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa vichocheo kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).

-Hyperthyroidism - Kukua kwa ukubwa wa tezi la koo na hivyo kutengeneza kwa wingi kichocheo aina ya thyroxine.

- Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi -Nusu ya wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa matiti kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini.

-Matatizo ya Ini -  Dawa za kutibu magonjwa ya kwenye Ini kama kuoza kwa ini, ini kushindwa kufanya kazi husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana kwa uwiano sawa wa mfumo wa vichocheo mwilini.

-Utapiamlo, ukame - Utapiamlo, ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa kichocheo aina ya testerone na kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa vichocheo mwilini. Hii hutokana na kukosekana kwa virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa  mbalimbali pamoja na tatizo hili.

-Madhara ya dawa za kurefusha maisha(ARVs) kwa wagonjwa wa Ukimwi.

-Utumiaji wa  dawa za kulevya kama bangi/ marijuana.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: