MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA ENEO LA UBUNGO MAJI JIJINI DAR

 Wasamalia wema wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka barabara. 
Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa  linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi. Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali. 
Mwili wa dada huyo akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema baada ya kukutwa umaiti.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.
Mmoja wa mashuda wa ajali ameiambia blog hii ya Pamoja kuwa mama huyo alipogongwa na daladala lá inayofanya kazi zake kutoka Mbezi - Muhimbili alafu likamburuza yapata mita kumi na tano, baada ya daladala kusimama yule mama akawa anajitahidi kutoka pale uvunguni  lakini ilishindikana na damu zilikuwa zinavuja kichwani. Mpaka walipo shuka abiiria wote waliokuwa wamepanda daladala hiyo na kuliinua na kumtoa mama huyo kwenye daladala ,na baada ya kutokea ajali hiyo dereva wa daladala hiyo alikimbia. Na mwanamke huyo amefariki papo hapo maana alitokwa damu nyingi kichwani na mwili wake umepelekwa  hospitali ya Muhimbili.

No comments

Powered by Blogger.