Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, jana alifanikiwa kudhibiti kuchafuka
hali ya hewa bungeni baada ya wabunge kutoka Zanzibar kutaka kumpiga Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy, (pichani)
wakichukizwa na kauli yake waliyoitafsiri kuwa ni ya kuikejeli
Zanzibar.
Keissy, ambaye mara kwa mara amekuwa akijikuta akiingia katika msuguano
na wabunge kutoka Zanzibar, alitoa kauli hiyo akipinga kauli ya Mbunge
wa Viti Maalum (CUF), Rukia Kassim Ahmed, aliyoitafsiri kuwa ni ya
kukejeli hatua ya Rais Jakaya Kikwete kwenda kutibiwa Marekani.
Rukia alitoa kauli hiyo katika mwongozo wa spika aliouomba bungeni jana chini ya kanuni ya Bunge ya 47 (1), (2) na (3).
Alisema kutokana na serikali kudaiwa na Bohari ya Dawa (MSD) Sh. bilioni
102, hali imekuwa mbaya katika hospitali nchini, wagonjwa wanateseka,
dawa hakuna, huku wabunge wakiendelea kupulizwa na viyoyozi bungeni na
Rais Kikwete akiwa nje ya nchi kuchunguzwa afya yake.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KBOFYA HAPA CHINI
“Kutokana na Serikali kudaiwa bilioni 102 na bohari ya madawa MSD hali ya
Hospitali zetu ni mbaya sana.. wagonjwa wanaendelea kuteseka na
maradhi, madawa hamna.. wanawake wanakufa, watoto wanateseka.. huku sisi
waheshimiwa wabunge tukiendelea kukaa humu tukila viyoyozi
"Kwa
taarifa tulizonazo Mheshimiwa Rais yupo nje kaenda kuchekiwa afya yake..
Ili tuwatendee haki Watanzania waliotuweka katika bunge hili na tuweze
kuokoa maisha yao naomba bunge lako liahirishe shughuli zinazoendelea
tuweze kujadii jambo hili kwanza.. tulipatie ufumbuzi kwa maslahi ya
Watanzania.. na kwa maana hiyo naomba kutoa hoja na waheshimiwa wabunge
naomba mniunge mkono..”-Rukia
Baada ya mwongozo huo wa Rukia , Keissy, alisimama na
kusema Rukia hakupaswa kulinganisha hoja yake na Rais Kikwete kuwapo nje
ya nchi kupatiwa matibabu na kuhoji kama alistahili kwenda kutibiwa
Zanzibar.
Keissy alisema anawajua baadhi ya wabunge wa CUF, ambao wamekuwa
wakienda mara kwa mara India kutibiwa na kusema iweje Rukia azungumzie
habari za Rais Kikwete kwenda kutibiwa Marekani.
“..Wabunge
wangapi wa upinzani tayari wameshawahi kwenda India mara sita.. Kwa
majina nawajua tena wa CUF wamekwenda India kutibiwa mara tatu mara nne
leo mnazungumzia habari ya Rais kwenda kutibiwa Marekani, aende kutibiwa
wapi Zanzibar? Acheni mambo yenu hayo.!.”-Kessy
Kauli ya Keissy iliwafanya wabunge kutoka Zanzibar kuhamaki na kuinuka
na kutaka kumpiga. Hata hivyo, Ndugai alisimama na kuwasihi
watulie na kuepuka kutoa kauli zinazoweza kuchafua hali ya hewa bungeni.
“..Waheshimiwa
wabunge ningewaomba sana kuhusiana na masuala ya wagonjwa wetu
mbalimbali wawe ni wabunge.. Awe ni mheshimiwa Rais na wanatibiwa wapi..
Naliomba jambo hili tuliache litatuharibia hali ya hewa bila sababu
jamani.. Nawaombeni sana hilo nimelitoa katika utaratibu na kwenye
hansard tulifute jamani..”-Job Ndugai
Wakati Ndugai akiendelea kuongea, Keissy alisimama na kuondoka katika
ukumbi wa Bunge. Baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar walimfuata Keissy,
lakini wakashindwa kumfikia kutokana na kusindikizwa na askari wa Bunge.
SOURCE: THE GUARDIAN



No comments:
Post a Comment