Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Kikundi
cha Wakulima cha Umoja Rika wakiinua majembe juu kama ishara ya
kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyefika
kwenye shamba hilo la ushirika la Mkotokuyana wilaya ya Nachingwea.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wa
kikundi cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana ,Nachingwea.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakulima wa kikundi
cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana,Nachingwea mkoani Lindi.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha treka kulima shamba la
ushirika la Mkotokuyana huku akiwa amempakia Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea Ngugu Mathias Chikawe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la Mkotokuyana wilayani Nachingwea.

Sehemu ya shehena ya Korosho.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia korosho kwenye
ghala ambalo hapo awali ilikuwa kiwanda cha korosho cha Nachingwea .

Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta Ilulu Nachingwea ambacho sasa kinatumika kama ghala ya kuhifadhia vifaa vya umeme.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Mandai ambao walieleza shida ya maji,zahanati pamoja na ofisi ya
Serikali .

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jiko
la kisasa la shule ya sekondari ya Nachingwea High School .

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majiko ya kisasa ya shule ya sekondari ya Nachingwea.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Nachingwea.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Naipanga ambapo alikagua na kushiriki ujenzi , Katibu mkuu wa
CCM aliwaambia wananchi wawe mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo
yao.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiongozana na Mbunge
wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani Ndugu Mathias Chikawe
(kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea Ndugu Albert
Mnari kuelekea kwenye shamba la ushirika Mkotokuyana wilaya ya Lindi
Vijijini tayari kwa kushiriki shughuli za kilimo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Naipanga Nachingwea.

Wananchi
wa Nachingwea wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha
chama mkoani Lindi.

Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo
aliwaambia upinzani umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao
kushabikia

Wananchi wakifurahia hotuba ya Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Mama akichukua matukio kwa simu yake wakati mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Soweto wilaya ya Nachingwea.

Wananchi wakifuatilia mkutano nje ya senyenge ya uwanja wa mikutano wa Soweto wilayani Nachingwea.

Mbunge
wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani akielezea
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika jimbo lake kwenye
mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, Nachingwea.

Bibi
Esha Kanduru mwenye umri wa 89 ambaye alishiriki harakati za uhuru na
kujiunga na TANU mwaka 1957 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Soweto,
Nachingwea.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa
Nachingwea ambapo aliwaambia kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali
inapokosea mambo na kuchelewa kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso
wanapata wananchi, akizungumzia kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya
korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa maghala na hakuna mtu serikalini
amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea Ndugu Mathias Chikawe wakati wa mkutano wa CCM mjini
Nachingwea kwenye viwanja vya Soweto.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachma
kutoka CUF waliojiunga rasmi na CCM wilayani Nachingwea.



No comments:
Post a Comment