Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Polisi
nchini Ufaransa wameeleza kuwa hali mbaya ya hewa itakwamisha zoezi la
utafutaji miili ya watu wapatao mia moja na hamsini katika eneo la ajali ya
ndege na hivyo kuchukuwa siku kadhaa. Siku ya jana ndege ya Ujerumani
ilianguka katika eneo la milima ya Alps huko Ufaransa nakuua watu wote wapatao
mia moja na hamsini waliokuwemo.
Waathirika wa ajali hiyo
wanatoka nchi mbali mbali ambapo arobaini na tano ni wahispania huku zaidi ya
sitini wakiwa ni wajerumani.Kumi na sita, kati yao walikuwa ni wanafunzi kutoka shule
moja nchini Ujerumani ambao walikuwa wakijerea kutoka katika ziara ya
kutembelea Hispania.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Pierre-Henry Brandet msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani amewaambia
waandishi wa habari kwa zoezi la kuuopoa na kutambua miiili ndio kinachoopewa
kipau mbele.
"Kipaumbele chetu ni kupata miili mingi kwa kadri tuwezevyo ili
kuwafanya wataalam wa utambuzi wa uhalifu waweze kuifanyia utambuzi.
Na sio miili
pekee kitu chochote ambacho kitatusaidia kuitambua miili kama vile mizigo ya
abiria ambayo atakuwa ameibeba itachukuliwa na itatuwezesha kuupeleka mwili katika nchi aliyotoka lakini ni mapema kusema ni wakati
gani."
Naye Raisi wa Marekani Barack
Obama amesema kwamba taifa lake linaungana na mataifa ya Ujerumani na Hispania
katika kipindi hiki kigumu walichopotezawapendwa wao."Nataka
kusema kwamba mawazo na sala zetu tunazielekeza kwa marafiki zetu walioko Ulaya
,na hasa kwa watu wa nchi za Ujerumani na
Hispania ,kufuatia ajali mbaya
ya ndege iliyotokea nchini Ufaransa.Inaumiza kwa sababu ajali hiyo
imepoteza watoto wengi kwa wakati mmoja ,na walio wengi watoto
wachanga.nilimpigia simu kansela wa Ujerumani Angela
Merkel natarajia kuongea na
Raisi ama waziri mkuu wa Hispania Rajoy baadaye leo kutoa salamu za rambi rambi
kutoka kwa watu wa Marekani ,lakini pia kutoa msaada wowote
utakao hitajika wakati huu wa uchunguzi wa chanzo cha ajali iliyosababisha
janga kubwa.."
No comments:
Post a Comment