Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mhariri mkuu wa Bongo5 Bw. Fredrick Bundara akiwa pamoja na mwariri msaidizi, Sandu George wakizungumza leo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tuzo za watu 2015
Kampuni ya Bongo5 Media Group, imezindua msimu mpya na wa pili wa Tuzo za
Watu Tanzania zilizoanzishwa mwaka jana ili kuwatuza watu kwenye sekta ya
burudani na habari wanaofanya vizuri.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa
habari leo, mhariri mkuu wa mtandao wa Bongo5, Fredrick Bundala amesema tuzo za
mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuongeza vipengele vitatu vipya.
“Mwaka huu tuzo zimeongezewa nguvu
zaidi. Kutoka vipengele 11 tulivyokuwa navyo mwaka jana hadi vipengele 1. Mwaka
huu tumeongeza vipengele vitatu muhimu,” amesema Bundala.
Amevitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa
ni pamoja na muongozaji wa filamu anayependwa, tovuti/blogu inayopendwa na
mfadhili maarufu anayependwa.
“Kwenye jamii yetu kuna watu maarufu
ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hususan watu wasio na uwezo ama
wanaoshi katika mazingira magumu. Tumeona ni muhimu pia kuwatambua watu hawa
ambao huamua kujinyima na kugawana kile wanachokipata ili kuwasaidia watu
wanaohitaji msaada,” ameongeza.
Amesema zoezi la kuanza kupendekeza
majina ya washiriki limeanza rasmi Alhamis hii ambapo wananchi wanaweza
kuwapendekeza kupitia website ya www.tuzozetu.com
ama kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu kwa kuandika neno TZW, code ya kila
kipengele na jina la anayependekezwa kwenda 15678.
“Baada ya wiki tatu kuanzia leo
tutatangaza majina ya washiriki watano waliochaguliwa kuingia kwenye awamu ya
kwanza ya mchujo ambapo katika kipindi cha wiki mbili itafanyika michujo
mingine miwili ili kuwapata washiriki watatu watakaoingia fainali,” amesisitiza
Bundala.
“Washiriki watatu kwenye kila kipengele
watahudhuria kilele cha tuzo hizo kitakachofanyika katikati ya mwezi wa tano.”
Kwa upande wake mhariri msaidizi wa Bongo5, Sandu Mpanda, amesema kuwa utofauti wa tuzo
za watu na tuzo zingine ni kuwa wananchi wana nguvu ya asilimia 100 kumchagua
mshindi.
No comments:
Post a Comment