Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kampuni ya Boti za Azam Marine Zanzibar yatowa Boti Mpya ya Kilimanjaro V,iliowasili juzi katika bandari ya Zanzibar na inategemewa kuaza kutoa huduma ya Usafiri kati ya Zanzibar na Dar-es-Salaam mwishoni mwa wiki hii baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria na kuaza kutowa huduma hiyo. Ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo.Ina uwezo wa kuchukua Abiria 550, inachukua masaa maskamu saa moja na nusu mpaka Dar.
Sehemu ya VIP kama inavyoonekana
Sehemu ya VIP One ikiwa na Video katika viti vyake vyenye uwezo wa kulala wakati abiria wakiwa safarini.
Kepteni wa Boti Mpya ya Kilimanjaro V Thomas Buhatwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar kuhusiana na huduma zinazopatikana katika boti hiyo mpya na kutowa maelezo ya vyombo vya kisasa vilivyomo katika boti hiyo wakati wa kuitembelea boti hiyo ikiwa katika bandari ya Zanzibar.
Kapteni Thomas Buhatwa akionesha mitambo ya kisasa ya boti hiyo inayoonesha hali halisi ya bahari wakati wa safari zake akiwa katika chumba cha makepteni katika biti hiyo wakati waandishi walipotembelea biti hiyo mpya.
Meneja Mkuu wa Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar V wakati waandishi hao walipoitembelea Boti hiyo Mpya na kupata maelezo kutoka kwa Meneja, Boti hiyo ikiwa katika bandari ya Zanzibar na kuelezea ina uwezo wa kuchukua abiria 550 kwa wakati mmoja na mizigo pia amesema ina uwezo wa kusafiri kati ya Zanzibar na Dar kwa muda wa saa moja na nusu, Amesema inatarajiwa kutoa huduma mwishoni mwa wiki hii ikikamilisha taratibu zote zilizobaki katika vyombo husika.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na Mwakilishi wa kampuni ya RDM- Marine Engineer ya Australia Egn Kerry Williams, wakiwa katika boti hiyo baada ya ukaguzi na majaribio ya Boti hiyo yaliofanyika hadi katika visiwa vya Chumbe na kurudi baada ya ukaguzi uliofanywa na ZAM.
No comments:
Post a Comment