Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Ofisa Uratibu na Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Genoveva Vicent (kulia), akimuelekeza jambo mwananchi aliyetembelea banda la NHIF katika maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya Manazi Mmoja Dar es Salaam jana. Wengine wa pili kushoto ni Ofisa wa NHIF, Ambrose Manyanda na Ofisa Mawasiliano wa NHIF, Luhende Singu.
Mtaalamu wa Maabara wa Hospitali ya Amana, Johnbosco Kishebuka (kushoto), akimpima urefu mwananchi aliyefika katika banda la NHIF kabla ya kufanyiwa vipimo vingine.
Mwanahabari Beatrice Mbwambo (kulia), ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kupima afya yake katika banda la NHIF ambapo huduma hiyo ya kupima ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na , saratani ya matiti.
Ofisa wa NHIF (kushoto), akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika kwenye banda la NHIF.
Wananchi waliotembelea banda la NHIF wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa maofisa wa NHIF.
Wananchi wakiwa wamefurika banda la NHIF kwa ajili ya kupata huduma za kupima afya zao.
Wadau mbalimbali wakisubiri kupata vipimo katika banda la NHIF. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)



No comments:
Post a Comment