Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Naibu Katibu Mkuu Nassor Ahmed Mazurui alipozungumza na waandishi
wa habari (picha kutoka Maktaba)
Na Talib Ussi, Zanzibar
CHAMA cha wananchi CUF kimewapongeza wanachama na wale waliowaita
wazalendo wa nchi yao ya Zanzibar kwa kukubali ushauri wa chama hicho wa
kususia uchaguzi wa marejeo kiliodai ni Batili.
Kauli ya chama hicho imetolewa na naibu Katibu Mkuu Nassor Ahmed
Mazurui alipozungumza na waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Vuga
Visiwani hapa. Alisema kukataa huko kwenda kupiga kura wameidhihirishia
Dunia kwanjia ya amani na ya ustarabu kuuwa chaguo lao ni Maalim Seif
sharif Hamad kuiongoza Zanzibar.
“Kwa mara nyengine tena Wazanzibar wameyathibitisha maamuzi yao ya
Kidemokrasia waliyoyafanya kupitia uchaguzi huru na wa haki wa 25 octoba
mwaka jana”, alisema Mazurui. Alisema kutokana na hilo hawatambui uchaguzi wa marejeo wala
hawatashirikiana wala kuitambua Serikali itakayoundwa kutokana na kile
walichokiita matokeo batili.
“Chama chetu sisi kilishaeleza mapema msimamo wetu kwa hiyo hili la
kuatoa mchango wowote kwa uchaguzi huu haramu halipo” alisema Mazurui.
Kupitia nafasi hiyo mazurui alivipongeza vyombo vya habari vya nje
na ndani kwa kile alichokisema kuonesha hali halisi ilivyokuwa na jinsi gani
wanzibar walivyoikataa CCM na watawala waliobaka demokrasia.
“Wazanzibar wameandika historia nyengine mbele ya macho ya
ulimwengu na kwa mara nyengine Wazanzibar wameshindaa” alieleza Mazurui.
Alisema chama kinajua kwamba wazanzibar wanahamu ya kujua ni hatua
gani zinafuata katika kusimamia maamuzi yao ya kidemokrasia waliyoyafanya 25
October mwaka huu.
“Nina waambia wananchi kwamba, Chama chao hakijayumba na wala
musiwe na ghofu na kinafuatilia haki yao kwa njia za amani na za kidemokrasi na
kitakuwa kiinatoa maelezo kwa kila kinachoendelea” alieleza Mazurui.
Chama cha wananchi CUF hakikushiriki uchaguzi wa marejeo kwa madai
kwamba uchaguzi huo ni batili.
No comments:
Post a Comment