HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KAMA UNATAKA KUFANIKIWA UNAHITAJI TU KUJUA HIZI NJIA SABA(7)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Iwe unataka kuwa mwanafunzi bora, mtafiti mahiri, mzazi hodari au mjasiriamali aliyefanikiwa sana, lazima utakuwa na namna ile ile ya unavyofikiria. Haya ni miongoni mwa mambo unayohitaji kuyazingatia kuhakikisha kuwa unakuwa bora.

1. Weka malengo ya kukuimarisha
Kama una malengo madogo ni ngumu kuwa bora. Weka malengo yako siku zote kwenye akili yako na utahisi kuimarika. Sio mbaya kuyaandika. Unajua pia uwezo wako na huo ndio ufunguo. Lazima pia kuwe na dozi ya afya kujikosoa mwenyewe. Nini udhaifu wako? Unaweza kupata ujuzi mpya kukabiliana nao?

2. Kamwe usisahau thamani na maadili yako

Yote kwa yote, fahamu kuwa thamani na maadili fulani siku zote huwa msingi wa kuwa bora. Hutaibia mtihani, hutawekeza kwenye biashara chafu. Uaminifu, usawa na maadili ni vitu muhimu katika kuutafuta ubora.

3. Unaweza kukabiliana na vikwazo
Soma kitabu chochote unachotaka cha historia za mafanikio kuanzia Albert Einstein, Nelson Mandela, Steve Jobs hadi Bill Gates. Wote walikuwa na kitu kimoja kinachofanana. Walikutana na vikwazo na kufeli lakini hawakukata tamaa.

4. Una nidhamu
Unajua hatua gani unatakiwa kuzichukua kufanikisha mambo. Weka malengo yako ya kila siku kwenye ngazi inayokuongoza kwenye kilele utakakotuzwa. Hiyo inahitaji kujitoa, kufanya kazi kwa bidii, uvumilivu na hakuna njia za mkato.



5. Unatengeneza marafiki, sio maadui
Katika ulimwengu ngangali wa biashara na mbio za panya, unaweza kushawishika kutafuta kulipiza kisasi. Matokeo yake sio mazuri na yatakuathiri. Ukarimu utakusaidia na watu wako wa karibu. Maadui hawatakupigia simu ila marafiki watafanya hivyo.

6. Unajua jinsi ya kuwekeza kwenye muda wako

Matumizi ya muda yanasaidia. Vitabu vingapi unahitaji kusoma ili kujiimarisha kwenye kazi yako? Unapataje muda wa kuvisoma vyote? Teknolojia inaweza kukusaidia kuwa bora. Kuna apps zinazoweza kukusaidia kila unachotaka kujua kwa ufupi kwenye vitabu mbalimbali.

7. Unajua jinsi ya kuweka usawa kati ya kazi na maisha mengine

Katika kutafuta furaha, watu wengi husahau mambo mengine muhimu katika maisha yao. Kazi inachukua asilimia 95 ya maisha yao. Lakini kwa mabadiliko kidogo, unaweza kubadilisha ubora wa maisha yako na kupata usawa wa kazi na maisha.
Mtazame Nigel Marsh akielezea baadhi ya mabadiliko hayo.
Inabidi uamue kuwa bora. Kutakuwa na maamuzi mengi ya kufanya kufikia hapo. Muhimu zaidi umepata muongozo wa kuishi maisha bora wakati ukiendelea na safari.
By Robert Locke – Life Hack

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: