Faustine Munishi(malebo)(Kushoto), Moses
Kulola(katikati) na Emmanuel Mwasota(kulia).
MOSES KULOLA, alizaliwa mwaka 1928
katika familia ya watoto kumi, na kufariki mwezi Agosti
2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway
jijini Dar es Salaam. Ambapo kwa sasa wamebaki ndugu zake wanne.
Moses Kulola alijiandikisha katika shule ya
kwanza mnamo mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ilikiwa ni
shule ya Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School, Moses Kulola akajiunga katika Idara ya Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka
1949. Na mwaka 1950 alibatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza.
Alifanikiwa kumuoa Elizabeth na Mungu aliwajalia kupata
watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai. Alianza kazi za
Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa alikuwa amesikia wito huo mwaka ule wa
1949.
Mwaka 1959 aliajiriwa serikalini. Lakini pamoja
na kuajiriwa huko Moses Kulola aliendelea na kuhubiri Injili katika Miji na
Vijiji. Utumishi wake kama mwajiriwa wa Serikali ulikwisha mwaka 1962 baada ya
kuwa amekabidhi nguvu, mwili na nafsi yake katika kazi ya Mungu! Ilipofika
mwaka 1964 aliamua kusoma na akajiunga
katika Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha Diploma mamo
mwaka ule wa 1966.
Baada kupata Diploma hiyo hakuishia hapo bali aliendelea kusoma kwa Njia ya
Posta na kupata Vyeti vingi sana kutoka Sehemu mbali mbali duniani.
Alitumikia miaka miwili kama mchungaji,
1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo akawa muumini wa
Kipentekoste. Halafu akatumikia katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi 1991
ambapo alijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu kama EAGT.
EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa nchini hasa Tanzania,
Zambia na Malawi ambapo jumla yake ni kama makanisa 4,000 yakiwa ni makanisa
makubwa na madogo, na yeye Moses Kulola ndiye akiwa Askofu Mkuu na Msaidi wake akiwa Askofu
Mwaisabira.
Ilikuwa sio kazi rahisi kuendesha makanisa
elfu nne (4,000) na ndiyo maana ikabidi Moses Kulola kuamua kugawanya makanisa
hayo katika maeneo 34 ya kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi
hiyo ya Mungu. Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.
R.I.P ASKOFU MOSES KULOLA

No comments:
Post a Comment