Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamepongeza juhudi za wanamichezo wa Tanzania wanavyoiwakilisha vyema Tanzania hasa katika mambo mbalimbali ikiwemo Michezo kama alivyofanya Bondia Francis Cheka.
Akitoa pongezi hizo mapema leo, Waziri wa Habari,  Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na bondia huyo pamoja na viongozi wa soka akiwemo Rais wa chama cha Ngumi pamoja na Promota wa bondia huyo, Waziri Nape ameelezea kuwa kadri wanamichezo wanavyofanya vizuri ndiyo wanavyoendelea kuipa sifa kemkem nchi hivyo wataendelea kushirikiana nao.
Mbali na kumpongeza bondia, Francis Cheka, Waziri Nape pia alimpongeza mdogo wa bondia huyo Francis Cheka, Cosmas Cheka ambaye naye aliambatana na msafara huo ambapo katika pambano lake naye alishinda mkanda wa WBF, kwa pointi dhidi ya mpinzani wake.
Aidha, Waziri Nape  alimkabidhi cheti cha shukrani bondia, Cheka kama ishara ya kutambua mchango wake huo na kuiletea heshima Taifa kwa ushindi wake.
Bondia,  Francis Cheka katika pambano lake hilo, alipigana na Raia wa Serbi anayeishi Marekani, Bondia, Geard Ajetovic ambapo katika pambano lao hilo, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Cheka alishinda kwa pointi.
Ubingwa huo alioshinda Bondia Francis Cheka, ni Ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF).
Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa:
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv



 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment