Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Staa wa muziki Shetta amesema alichokifanya Nay wa Mitego kwenye wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ni kama kichekesho kwake.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Shetta amesema yeye na Nay ni washikaji.
“Hiyo kwangu ni kama kichekesho sababu huyo Nay wa Mitego mwenyewe anajua alichofanya ni kama kichekesho kwangu siyo issue ya kufanya mimi nikachukulia kama tatizo sababu ukweli wote hata yeye anajua, sisi ni kama familia ndiyo maana unaona mimi nimepost video yake. This is my car ndiyo maana yeye kasema hajui labda muulize Shetta sababu yeye hajui” Alisema Shetta
Pia Shetta amesema yeye mbali na muziki ni mfanyabiashara hivyo anapata maendeleo na pesa za kutosha ndio maana anaweza kumiliki gari kama hiyo.
“Mimi nafanya mitikasi yangu, mfanyabiashara na mwanamuziki hivyo napiga show za kutosha na bado na hustle sana hivyo na kila sababu ya kupata maendeleo na maendeleo ndiyo haya sasa, hivyo sioni kama ni tatizo na wala sioni kama amenisema kwani nilikuwa najua toka before lakini pia mimi ndie mwenye mamlaka ya kila mtu na hakuna mtu mwingine mwenye
No comments:
Post a Comment