Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars),
leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya
Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania
kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa
Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma
imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika
uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake
wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF uliopo
Karume, Nasra amesema ana waheshimu Zimbabwe wana timu nzuri, ndani ya
miaka minne wameshacheza nao zaidi ya mara nne, mapungu yaliyojitokeza
katika michezo iliyopita wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani
watafanya vizuri.
Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho
Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars
katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za
Afrika Mashariki.
Naye nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote
wapo katika hali nzuri, wana ana ari na morali ya hali ya juu kuelekea
kwenye mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti kwa
kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia uwanjani watakapokuwa
wakipeperusha bendera ya Tanzania.
Wapinzani wa Twiga Stars, timu ya taifa ya Zimbabwe wanawasili leo
jioni tayari kwa mchezo huo, huku waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini
Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la
Kenya (KQ).
No comments:
Post a Comment