Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
RC wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3.
RC wa Dodoma Jordan Rugibana akiteta na Mkuturenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, wakati wa uzinduzi.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa Mradi wa PS3 mkoani humo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, akitoa mada kwenye uzunduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais (Utumishi) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
Matiko Machonchoryo wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Dodoma siku ya Jumanne
na Jumatano, Machi 22-23, 2016.
Mradi
huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni
wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97
katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3
inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za
umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa
taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya
Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya
kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo
hazijanufaika vya kutosha.
Katika
uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana,
na uzinduzi
ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa
Songwe, Chiku Galawa. Watu takribani 180
walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa
ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri,
Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye
Halmashauri.
Mkoa
wa Dodoma una Halmashauri nane, ambazo
ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri
ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri
ya Mji wa Kondoa.
PS3
ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.
Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo
ni: Abt Associates Inc., kama
mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa
(BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za
Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute,
Intra Health International, na Urban Institute.
Mikoa
13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera,
Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na
Shinyanga.
PS3
itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi
utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia
kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa
wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa
ni pamoja na:
· Utawala
Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji
wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili
kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika
kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.
· Rasilimali
Watu: Kuongezeka kwa usawa katika
mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo
yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa
ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.
· Fedha:
Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi
katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi
cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.
· Mifumo ya
Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.
Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua
changamoto na mikakati
ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo
na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi
serikalini.
No comments:
Post a Comment