HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » LEO KATIKA HISTORIA: UNDANI WA PAPA WEMBA HUU HAPA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu


Papa wemba alizaliwa Juni 14 mwaka 1949 katika eneo la Lubefu mkoani Sankuru katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Ukitaja wakongwe na wakali wa sauti barani Afrika usipomtaja mwanamuziki wa dansi kutoka Kongo, Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba ‘Papa Wemba’, utakuwa umekosea sana!
Wemba ni mkongwe katika sanaa na muziki lakini sauti yake tamu na nzuri bado iko vilevile licha ya umri kuonekana umemtupa mkono. 

KAtika historia yake ya kimziki alikuwa akiimba miondoko tofauti tofauti lakini mziki aliopendelea kuimba ni muziki wa miondoko ya Lese- Rhumba ambayo baadaye ilijulikana kama Soukous, Afro Pop Soukous, African Traditions na Central African.

Zipo nyimbo na albamu nyingi alizofanya miongoni mwao ni pamoja na Pauline alioufanya mwaka 1970 akiwa na Kundi la Zaiko Langa Langa mwaka 1995 aliachia albamu ya Emotion ikiwa na wimbo mkali wa Show Me The Way, mwaka 1996 alifanya Wimbo wa Wake-Up 1996 akishirikiana na Koffi Olomide, mwaka 2014 aliachia albamu ya Maître D’école-Teacher.
Nyingine ni Esclave, Maria Valencia, Lingo Lingo, Madilamba na Mwasi.
Wemba ni mwanamuziki maarufu sana barani afrika na hata duniani. Anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza walioanzisha Bendi ya Soukous Zaiko Langa Langa mwaka 1969 mjini Kinshasa akiwa na wanamuziki kama Nyoka Longo Jossart, Manuaku, Pepe Felly, Evoloko na wengineo.
Mwaka 1977 alianzisha Bendi ya Viva la Musica akiwa na vijana wenye vipaji kutoka kijijini kwao na kufanikiwa kuachia nyimbo kama Mere Superieure, Mabele Mokonzi, Bokulaka na zinginezo.

Mbali na uimbaji, Wemba pia ni muigizaji na alishawahi kushiriki katika filamu ya La Vie Est Belle- Maisha ni Bora iliyofanikiwa sana nchini Zaire (Kongo kwa sasa) mwaka 1987.

Mwaka 2003 alishukiwa kuhusika katika mtandao ambao inadaiwa walivusha mamia ya wahamiaji haramu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani Zaire) hadi Ulaya, Papa Wemba alikamatwa nyumbani kwake mjini Paris na kufungwa jela miezi mitatu na nusu na baadaye kuachiwa baada ya kutokupatikana na hatia, ndani ya mwaka huo aliachia albamu ya Somo Trop ikiwa na wimbo unaozungumzia kile kilichomkuta maishani mwake.
Mkali huyo wa sauti atakumbukwa hapa nchini Tanzania baada ya hivi karibuni alitua Bongo kwenye Tamasha la KARIBU MUSIC FESTIVALS 2015 lililofanyika Novemba 6, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na kuacha historia ya aina yake kutokana na kutozeeka sauti na kuonesha umahiri wa hali ya juu katika uimbaji.
Marehemu Papa Wemba amefariki tarehe 24 mwezi wa nne mwaka 2016 alipokuwa akitumbuiza katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan,
''Marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali. lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wake wa tatu Papa Wemba alianguka na kuzirai ghafla jukwaani'' Watu wa shirika la msalaba mwekundu walijaribu kumsaidia lakini hakuonesha dalili nzuru kwa hivyo wakampeleka hospitalini kwa dharura lakini baada ya dakika karibu thelathini hivi tukaambiwa kuwa Papa Wemba ametuacha''

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: