Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakitazama majina ya masanduku yaliyobeba miili ya marehemu, tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFGterM4Jr3-si6NN9PfkV7oBpPkp0b91iwluQrDM8tzapWIsWklgDcoBrrLV2CLdfIAq504gr35d-2YsVBxHeZwIKkTRGNVKyAUUhRqiZzRdFWENNf-U88l6CUCbAATH8UlUxa2M2jPWA/s640/DSC_0030.JPG)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.
Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.
Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.
![](https://scontent-bru.xx.fbcdn.net/v/l/t1.0-9/14264874_1118354961545985_3994046295947733095_n.jpg?oh=ca5cc0d8c82c2da48fdd584147414388&oe=58458A52)
Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.
![](https://scontent-bru.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/14332969_1118355954879219_1473751176491168191_n.jpg?oh=7a652809ecce2b6fa5ede1fc99f918f6&oe=58792FEF)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Mh Wilfred Lwakatare,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu, waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa na simanzi wakati wa kuagwa kwa miili ya wapendwa wao
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga wapendwa wao![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhP7S2mTvBUk2v2iWfMtz84cfmt1GDhSgKHkcfwlWArAPpfe-8XloD8Rij1acU67M0bjyS-TeDcaVRwp6uY3sC0mRRuJ4eIQVmzpJKJaTBCCdfTVE9he-DAzq9xzVSSX-b_SKEa4mB3bfh1/s640/DSC_0054.JPG)
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.
Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya marehemu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba Mkoani Kagera.![](https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif)
![](https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif)
Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Mh Wilfred Lwakatare akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa miili ya watu 16 waliofariki katika tetemeko la ardhi.
Meya wa Manispaa ya Bukoba akizungumza jambo
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini kitoa neno wakati wa kuagwa kwa miili 16
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Kagera
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waliofika kuaga miili ya wau 16 waliofariki kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Mh Wilfred Lwakatare akiwapungia mikono wananchi wa manispaa ya Bukoba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekonfari ya Ihungo baada ya madarasa na mabweni kuharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo. (Picha na Faustine Rutta)
No comments:
Post a Comment