HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » JE WATAKA KUJUA: MASHARTI YA KUPIGA PICHA UKIWA NCHINI KOREA KASKAZINI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Serikali ya Korea Kaskazini imeweka utaratibu maalum kwa wananchi na watalii wanaotembea nchi hiyo wanapotaka kupiga picha. 

Unapotaka kupiga picha sanamu au picha ya "viongozi wapendwa" wa nchi hiyo Kim Jong Il, Kim Il Sung na Kim Jong Un ni lazima upige picha sanamu zima au picha nzima, ni marufuku kupiga kipande au nusu picha. Ni marufuku pia kuchora katuni za viongozi hao.
Ukienda kwenye eneo la ujenzi ni marufuku kuwapiga picha wafanyakazi wanaoendelea na ujenzi wala kupiga picha jengo lisilokamilika, ni lazima upige picha jengo lililokamilika na lenye kupendeza.
Ni marufuku kupiga picha wanajeshi au kambi ya jeshi, hili ni sharti gumu kidogo kwasababu asilimia 25 ya raia ni wanajeshi.
Ni marufuku kutembea peke yako na kupiga picha maeneo yaliyoharibika kama vile barabara mbovu au maduka ambayo hayajajaa bidhaa. Serikali ya Korea Kaskazini inajitahidi ulimwengu upate picha ya kupendeza kuhusu nchi hiyo.

Imeandaliwa na Moses Mutente

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: