HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » JESHI LA POLISI LATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA MADEREVA WA BAJAJI JIJINI MBEYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya madereva wa pikipiki za magurudumu matatu, maarufu kwa jina la Bajaji ambao wamejaribu kufunga barabara kuu ya Tanzania na Zambia kupinga zuio la serikali la kutaka bajaji zisipite kwenye barabara kuu.

Shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Kabwe, Soweto na Block T jijini Mbeya yamegeuka uwanja wa vita baada ya jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana wanaodaiwa kuwa madereva wa bajaji ambao wamejaribu kufunga barabara kuu ya Tanzania kushinikiza bajaji ziruhusiwe kupita kwenye barabara hiyo inayounganisha Tanzania na nchi jirani ya Zambia.

Baadhi ya wananchi wamesema kuwa hakuna umuhimu wa polisi na madereva bajaji kusababisha uvunjifu wa amani na usumbufu kwa raia wema na badala yake suala hilo lingeweza kupata ufumbuzi mahakamani.

Akizungumza na ITV kwa njia ya simu, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Dhahir Athuman Kidavashari amesema kuwa mapema leo asubuhi jeshi hilo limewakamata vijana ambao ni madereva wa bajaji wapatao 22 na kuwafikisha mahakamani kwa tuhuma za kuvunja sheria za usalama barabarani lakini kundi la vijana ambao amedai kuwa ni vibaka wakataka kutumia mwanya huo kufanya vitendo vya uhalifu na ndipo polisi wakaamua kutumia nguvu kuwatawanya ili kulinda amani na usalama wa eneo hilo.

Kamanda Kidavashari amesema tayari jeshi hilo limewadhibiti vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwakamata baadhi yao, hivyo akawataka wananchi wema kuondoa hufu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: