Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kocha wa Ndanda FC, Hamimu Mawazo
KOCHA wa Ndanda FC, Hamimu Mawazo, amewachimba mkwara wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Simba, akiwataka wajiandae na matokeo ya kushangaza.
Ndanda itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo huo utakaochezwa Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Akizungumza jana, Mawazo, alisema haihofii Simba kwa kuwa wachezaji wake wana uwezo wa kuisimamisha timu hiyo inayoongoza ligi.
"Tumeanza mazoezi jana (juzi), lakini wachezaji wangu wengi walikuwa wakifanya mazoezi binafsi wakati ligi iliposimama, kwa sasa ni kuwapa mbinu ambazo naamini zitaisimamisha Simba," alisema Mawazo.
Alisema wekundu wa Mzimbazi hao wasitarajie mteremko kwenye mchezo huo wa Jumamosi.
"Simba watakuja kwa lengo la kutaka kujihakikishia wanaendelea kukaa kileleni, lakini na sisi pia tunahitaji pointi tatu zitakazotupandisha juu kwenye msimamo wa ligi," alisema Mawazo.
Alisema wanataka kuanza vizuri mzunguko wa pili wa ligi kwa kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza.
Simba inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35 huku Ndanda ikishika nafasi ya kumi ikiwa na pointi 19.



No comments:
Post a Comment