HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » RUSHWA YA NGONO IMECHANGIWA NA WANAUME KUTOKIDHI MAHITAJI NYUMBANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baadhi ya wanaume ambao wamekua wakiacha fedha kidogo kulinga na na mahitaji ya chakula nyumbani wamechangia ushawishi wa rushwa ya ngono kutoka kwa wanawake hao na dhidi ya wauzaji sokoni huku tamaa nayo ikiwa kichocheo cha rushwa hiyo.

Wakiongea katika mafunzo juu mapambano na mwanamke na rushwa ya ngono sokoni yanaendeshwa na Asasi isiyo ya Serikali(TAPEO) mkoani morogoro baadhi ya wafanyabishara wamesema wapo wanawake ambao wamekuwa wakienda sokoni na kutaka kupewa vyakula vingi na vitu vizuri ambavyo haviendani na kiasi cha fedha walionayo huku wakieleza kuwa kutokana na upungufu huo wa wafanya biashara wamekua wakijiingiza katika rushwa ya ngono.

Naye makamu mwenyekiti wa Asasi isiyo ya kiserikali (Tapeo) Abdallah Kazembe amesema kuwa rushwa ya ngono imeongezeka kwa wanawake wafanyabiashara pale wanapohitaji mitaji ya kuendeleza biashara zao huku tamaa ya baadhi ya wanawake kupenda vitu vizuri kuliko uwezo wao na marejesho ya mikopo mbalimbali nayo imekua chachu ya ongezeka ya rushwa ya ngono maeneo ya masoko.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: