Mshambuliaji raia wa Gabon
Pierre-Emerick Aubameyang ameifungia Borussia Dortmund goli la mkwaju
wa penati la dakika za mwisho katika siku ya mwisho ya msimu wa Ligi
ya Bundesliga na kuwa mfungaji anayeongoza kwa kufunga magoli 31.
Katika mchezo huo wa jana Aubameyang
alifunga magoli mawili wakati Dortmund ikiifunga Werder Bremen 4-3,
goli lake la kwanza akilipata dakika tatu kabla ya mapumziko na la
pili katika dakika ya 89.
Aubameyang anakuwa mchezaji wa pili
kutoka Afrika kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu nchini Ujerumani,
baada ya Mghana Tony Yeboah kutwaa tuzo hiyo mara mbili wakati
akiichezea timu ya Eintracht Frankfurt katika msimu ya 1992-93 na
1993-94.
Pierre-Emerick Aubameyang akibusu tuzo yake ya ufungaji bora
Pierre-Emerick Aubameyang akipongezwa na wachezaji wenzake kwa kutwaa tuzo hiyo
No comments:
Post a Comment