Rais wa Marekani Donald Trump
anatarajiwa kuelezea umuhimu wa kukabiliana na itikadi kali katika
Uislam wakati akitoa hotuba yake nchini Saudi Arabia baadaye hii leo.
Hotuba yake hiyo katika mkutano wa
viongozi wa dini, anatoa ikiwa ni katika siku yake ya pili katika
ziara yake ya kwanza nje ya Marekani tangu awe rais.
Inaelezwa kuwa atajaribu kufanikisha
makubaliano ya ushirikiano wa kuimarisha kuungwa mkono Marekani
katika vita dhidi ya wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam (IS).
Hapo jana Marekani ilitia saini
makubaliano ya kibiashara yenye thamani ya dola bilioni 350 na Saudi
Arabia.
Rais Donald Trump akiwa na mwenyeji wake Mfalme Salman wa Saudi Arabia
No comments:
Post a Comment