Cristiano Ronaldo amesababisha
furaha kwa mtoto mlemavu aliyekuwa akiwasindikiza wachezaji wa Ureno
uwanjani akiwa kwenye kiti cha matairi katika mchezo wa Kombe la
Shirikisho dhidi ya Urusi.
Kapteni huyo wa Ureno alimfanya
mtoto huyo wa kike uso wake kujawa na tabasamu kubwa wakati alpokuwa
akiingia naye uwanjani kutoka kwenye lango la kuingilia wachezaji la
katika uwanja wa Spartak Jijini Moscow.
Katika hali ambayo iliamsha hisia za
wengi ni pale wachezaji wa Ureno wakijiandaa kwa wimbo wa taifa
Ronaldo alimpa mtoto huyo jaketi lake la mazoezi na kisha akambusu
katika paji lake la uso.
Cristiano Ronaldo akimpa jaketi lake la mazoezi mtoto huyo mlemavu
Mchezaji nyoto wa Ureno Cristiano Ronaldo akimbusu kwenye paji la uso mtoto mlemavu






No comments:
Post a Comment